Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kompyuta yatoa msimamo EPL, Arsenal bado kidedea!

KOMPUTA Pict

Muktasari:

  • Chelsea ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Arsenal, Jumapili na hivyo wababe hao wa Stamford Bridge wanakabiliwa na mlima mrefu wa kupanda ili kukamatia tiketi hiyo ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: SHUGHULI imeshakuwa nzito. Chelsea itakosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa mujibu wa utabiri wa kompyuta maalumu, ambayo imefichua Liverpool ndiyo itakayomaliza kwenye nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Chelsea ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Arsenal, Jumapili na hivyo wababe hao wa Stamford Bridge wanakabiliwa na mlima mrefu wa kupanda ili kukamatia tiketi hiyo ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.

Bao la Jurrien Timber liliihakikishia ushindi Arsenal baada ya Piero Hincapie kujifunga na kuisawazishia Chelsea baada ya lile la kwanza la Gunners lililofungwa na beki wa kati, William Saliba.

Ushindi huo umeifanya Arsenal kufikisha pointi 64 na hivyo kutengeneza pengo la pointi kufikia tano dhidi ya wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa, Manchester City iliyokusanya pointi 59 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kwa utabiri wa kompyuta ya BETSiE, Arsenal italinda pengo hilo la pointi tano hadi mwisho wa msimu, hivyo kushinda taji lake la kwanza la Ligi Kuu England tangu mwaka 2004. Kwenye utabiri huo ni kwamba Arsenal itashinda mechi 25, sare tisa na vichapo vitano.

Hiyo ina maana, Arsenal itashinda mechi sita kati ya tisa zilizobaki na kwamba itapoteza mechi mbili.

Man City nayo imetabiriwa kwamba itashinda mechi sita zilizobaki na kupoteza mbili. Utabiri wa mechi nyingine kwenye Top Five ni kwamba, Manchester United itamaliza msimu kwenye nafasi ya tatu ikiwa imekusanya pointi 67, pointi moja juu ya Aston Villa itakayomaliza kwenye nafasi ya nne na pointi 66.

Kompyuta hiyo maalumu imetabiri kwamba Liverpool itapambana kumaliza kwenye nafasi ya tano na pointi 65 kitu ambacho kitawafanya kujikamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Hilo lina maana kwamba, Chelsea inayonolewa na kocha Liam Rosenior itamaliza ligi kwenye nafasi ya sita, pointi mbili nyuma ya Liverpool na hivyo haitakuwapo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Brentford, Fulham, Bournemouth na Everton zitakamilisha orodha ya timu 10 za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Kwenye vita ya kushuka daraja, kompyuta imetabiri kwamba timu saba zitaendelea kuchuana. Na kwamba kwenye hilo, Wolves, Burnley na West Ham United ndizo zitakazoporomoka kwenye Championship, huku Tottenham Hotspur itaokoka kwa kumaliza ligi kwenye nafasi ya 16 ikiwa na pointi 43. Nottingham Forest itamaliza msimu kwenye nafasi ya 17 ikiwa na pointi 40, pointi nne juu ya West Ham.

Kwa sasa, vita yote imebaki kwenye mbio za ubingwa, ambapo Arsenal itahitaji kuendelea kujitanua kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo kwa kuhakikisha inashinda mchezo wao wa Jumatano usiku dhidi ya Brighton. Kisha itacheza na Everton uwanjani Emirates kabla ya kuwakabili Man City kwenye fainali ya Kombe la Ligi, Machi 22. Kwa upande wa mahasimu wao, Man City watakipiga na Nottingham Forest uwanjani Etihad kabla ya kusafiri kuifuata West Ham inayopambana na hali katika kujikwamua na sakata la kushuka daraja.