Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha West Ham apewa mechi mbili

Majanga Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo Mhispaniola alinaswa na West Ham United alipokwenda kuchukua mikoba ya David Moyes mwishoni mwa msimu uliopita.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Julen Lopetegui ameripotiwa kwamba amepewa mechi mbili za kuamua hatima ya kibarua chake kwenye kikosi cha West Ham United.

Kocha huyo Mhispaniola alinaswa na West Ham United alipokwenda kuchukua mikoba ya David Moyes mwishoni mwa msimu uliopita.

Lopetegui, 58, amekuwa na mwanzo mbaya kwenye kibarua chake huko West Ham baada ya timu hiyo kushika nafasi kwenye 10 la chini kwenye msimamo.

West Ham United imeshinda mechi sita kati ya 19 ilizocheza kwenye ligi, huku matokeo yao ya mwisho ni yalikuwa ya kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool katika mchezo waliocheza nyumbani. Matokeo hayo yamezidisha presha kwa kocha huyo wa zamani wa Real Madrid.

Kinachoripotiwa ni kwamba bodi ya klabu ya West Ham imempa Lopetegui mechi mbili za kujiokoa kabla haijachukua uamuzi wa kumfuta kazi. Hiyo ina maana, Lopetegui atalazimika kupata matokeo mazuri kwenye mechi mbili za ugenini dhidi ya Manchester City na Aston Villa kwenye Kombe la FA.

Alinusurika kufutwa kazi baada ya kupata ushindi muhimu dhidi ya Wolves. Mechi hiyo ilikuwa ya vita kali maana hata Wolves nao kocha wao Gary O’Neil alikuwa kwenye presha kubwa ya kuhusu kibarua chake. Wote walinusurika kazi baada ya mechi hiyo, lakini siku sita baadaye, O’Neil alifutwa kazi baada ya kipigo kutoka kwa Ipswich Town.

Na sasa ripoti zinafichua kocha wa zamani wa Chelsea, Graham Potter yupo kwenye mkao wa utayari wa kwenda kuchukua mikoba ya Lopetegui. Kocha huyo Mwingereza, Potter amekuwa hana kazi tangu alipoondolewa huko Chelsea mwaka 2023 baada ya kuinoa timu hiyo kwa miezi minane.

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Edin Terzic na Mjerumani Roger Schmidt nao wanahusishwa na kibarua hicho cha kwenda kuinoa West Ham.