Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha AS Monaco ataja sababu Paul Pogba kutocheza

POGBA Pict

Muktasari:

  • Pogba, 32, awali alifungiwa miaka minne baada ya kukutwa ametumia dawa hizo.

MONACO, UFARANSA: KOCHA wa AS Monaco, Adi Hutter ameweka wazi sababu ya kiungo wao Paul Pogba kutokuwapo uwanjani licha ya kuwa huru kutoka kwenye adhabu ya matumizi ya dawa zinazozuiwa michezoni iliyoisha miezi mitatu iliyopita.

Pogba, 32, awali alifungiwa miaka minne baada ya kukutwa ametumia dawa hizo.

Hata hivyo, nyota huyo wa Ufaransa alikata rufaa na akapunguziwa adhabu hadi miezi 18.

Baada ya adhabu hiyo kuisha, Pogba alisaini mkataba na AS Monaco ya Ligue 1 Juni mwaka huu lakini hadi sasa  nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Juventus bado hajaonekana uwanjani.

Akizungumza Julai mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Monaco, Thiago Scuro, alisema: “Tunatarajia kumuandaa kwa miezi mitatu kabla hajaonekana kiwanjani. Michezo ya kiwango cha juu inategemea sana sayansi na si jambo rahisi kwake kucheza kwa sasa. Monaco ni moja ya timu zenye kasi kubwa zaidi Ligue 1 na aina yao ya mchezo inahitaji mchezaji awe fiti kabisa.”

Sasa, kocha wa Monaco, Adi Hutter, amesema kuwa Pogba yuko karibu kurejea kwenye hali nzuri ya kucheza na anaendelea vyema na ratiba za mazoezi alizopewa na klabu.

Pia ameelezwa kuwa Pogba hataharakishwa kurudi uwanjani licha ya Monaco kukabiliwa na tatizo la wachezaji wengi kuumia.

Hutter alisema: “Hatuwezi kulinganisha hali ya Paul Pogba na ile ya Ansu Fati. Fati ni kijana zaidi kuliko Paul. Ansu amekuwa akifanya mazoezi kwa muda mrefu akiwa na timu kabla ya kuwa hapa. Naona watu wengi wamekuwa wakiulizia kwanini hachezi, niseme tu, tupo katika taratibu zetu, tulimpa muda wa miezi mitatu kabla hajajiunga na kikosi rasmi. Anakaribia kujiunga na timu na ana afya njema kimwili na kiakili.”

Pogba anaweza kurejea dimbani baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa ya  Oktoba mwaka huu.