Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klose abariki Messi kuvunja rekodi yake

Muktasari:

  • Messi mwenye miaka 38, ameifungia Argentina mabao 13 katika Kombe la Dunia kupitia mashindano matano tofauti.

DALLAS, MAREKANI: SAA chache kabla ya Argentina  kuanza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026, mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani na kinara wa mabao wa muda wote wa mashindano hayo, Miroslav Klose, ametoa kauli iliyowashangaza wengi kwa kuonyesha wazi kuwa anatamani rekodi yake ivunjwe na Lionel Messi.

Messi mwenye miaka 38, ameifungia Argentina mabao 13 katika Kombe la Dunia kupitia mashindano matano tofauti.

Iwapo atafunga bao moja atafikia mabao 14 na kuifikia rekodi ya Gerd Muller katika nafasi ya tatu ya wafungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia.

Iwapo atafunga mabao mawili atafikisha mabao 15 na kuifikia rekodi ya Ronaldo Nazario katika nafasi ya pili.

Kama atafunga mabao matatu au zaidi yatamfanya afikie au kuvunja rekodi ya Klose ya mabao 16, ambayo ndiyo rekodi ya juu zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.


Klose ambariki Messi

Klose alisema hana tatizo lolote kuona rekodi yake ikivunjwa na Messi.

“Karibu kabisa kufanya hivyo. Mimi ni shabiki wake mkubwa, na nimekuwa hivyo siku zote.”

Mjerumani huyo pia alieleza kuwa mfumo mpya wa Kombe la Dunia wenye timu 48 na jumla ya mechi 104 unaongeza nafasi kwa wachezaji kufikia rekodi mbalimbali.

“Natumaini rekodi yangu itavunjwa katika mashindano haya. Kwa kuwa kuna timu nyingi zaidi, kuna mechi nyingi zaidi na hivyo nafasi nyingi zaidi za kufunga mabao.”

Klose pia aliongeza:“Natumaini Argentina na Ufaransa watafika mbali.”

Mbali na kumsifu Messi, Klose alimpongeza pia kocha wa Argentina, Lionel Scaloni.

“Nina heshima kubwa kwake. Tulicheza pamoja Lazio na alinisaidia sana kuifahamu mji huo. Sisi ni marafiki wazuri.”

Kuhusu Messi mwenyewe, Klose alisema kwa kifupi:“Messi ni jiniasi.”


Fursa nyingine

Baada ya kushinda Kombe la Dunia Qatar 2022 na kuvunja rekodi nyingi katika maisha yake ya soka, Messi sasa ana nafasi nyingine ya kuongeza ukurasa mpya katika historia yake.

Mbali na kutetea ubingwa wa dunia, anaweza kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia ikiwa atafanikiwa kufunga mabao manne au zaidi katika mashindano haya.


Ratiba ya Argentina Kundi J

Argentina itaanza safari yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa kucheza dhidi ya Algeria leo.

Baadaye watakutana na Austria  tarehe 22 Juni kabla ya kumaliza hatua ya makundi dhidi ya Jordan tarehe 27 Juni.

Mashabiki wengi wa soka duniani watakuwa wakifuatilia kwa karibu kuona kama Messi ataweza kuifikia au hata kuivunja rekodi ya kihistoria ya Klose katika Kombe la Dunia la 2026.