Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klopp na Van Dijk wahoji mapumziko ya dakika tatu

Muktasari:

  • Uholanzi ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa sare ya 2-2 dhidi ya Japan mjini Arlington, Texas, Juni 14, katika mchezo uliokuwa na presha na ushindani mkubwa kipindi cha pili huku kila timu ikiamini kuwa ilikuwa na nafasio ya kuibuka na ushindi.

LOS ANGELES, MAREKANI: WAKATI Fainali za Kombe la Dunia 2026 zikiendelea, nahodha wa Uholanzi Virgil van Dijk amekuwa mchezaji wa kwanza kupinga wachezaji kunywa maji mara moja kwenye kila kipindi akisema jambo hilo linaharibu ladha ya soka.

Uholanzi ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa sare ya 2-2 dhidi ya Japan mjini Arlington, Texas, Juni 14, katika mchezo uliokuwa na presha na ushindani mkubwa kipindi cha pili huku kila timu ikiamini kuwa ilikuwa na nafasio ya kuibuka na ushindi.

Van Dijk alifungua ukurasa wa mabao kwa kichwa baada ya mapumziko, kabla ya Japan kusawazisha kupitia Keito Nakamura dakika chache baadaye. Crysencio Summerville aliirejesha Uholanzi uongozini kwa bao zuri, lakini Daichi Kamada akaisawazishia Japan dakika za mwisho na mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Baada ya sare hiyo, Uholanzi sasa inaelekeza macho yake katika mchezo ujao dhidi ya Sweden utakaochezwa Juni 20, ikiwa na shinikizo la kutafuta ushindi wa kwanza wa makundi.

Break zaibua utata

Licha ya mchezo huo kuwa wa kuvutia zaidi kipindi cha pili, hoja kubwa baada ya mechi ilikuwa ni mfumo mpya wa vipindi vya maji unaotumika kila dakika ya 22 katika kila kipindi, bila kujali hali ya hewa.

Van Dijk alisema wazi kuwa mfumo huo unapaswa kuangaliwa upya kulingana na mazingira ya kila mchezo.

“Kwenda kunywa maji ni jambo la kuvutia, lakini si kitu ninachokipenda sana. Kwa watazamaji pia si vizuri. Kama joto ni kali basi ni sawa, lakini kila mechi inapaswa kuangaliwa kivyake na isiwe lazima kwa kuwa kuna mazingira mechi inaweza kuendelea bila kuwa na breki,” alisema nahodha huyo wa Uholanzi.

Kauli hiyo imeibua mjadala mpana, huku kocha wa zamani wa Liverpool Jürgen Klopp naye akiungana na wako soaji, akidai vipindi hivyo vinaharibu mtiririko wa mchezo. Klopp alieleza kuwa soka linazidi kugeuzwa kuwa “onyesho la matangazo”, akisema mapum ziko hayo ni kama “kuta zilizojengwa katikati ya mchezo ili matangazo yapite lakini siyo jambo la kuvutia hata kidogo”.


FIFA YATETEA

Kwa mujibu wa mpango wa FIFA, mapumziko hayo ya dakika tatu yanalenga kulinda afya ya wachezaji, hasa kutokana na hali ya joto kali inayoweza kujitokeza katika mataifa mbalimbali wakati wa mashindano, hivyo siyo jambo la kupigwa na yeyote kwenye mchezo wa soka kwa sasa.