Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Palmer, Manchester United yatajiwa pesa ya kuweka mezani

Muktasari:

  • Palmer amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea Manchester alikozaliwa na kucheza kwenye akademi ya ya Manchester City, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa na kubeba mataji ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kupewa dakika cheche za kucheza.

Manchester United imeonywa italazimika kuvunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza kwa dau la zaidi ya Pauni 150 milioni ili kumng’oa Cole Palmer Chelsea.

Palmer amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea Manchester alikozaliwa na kucheza kwenye akademi ya ya Manchester City, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa na kubeba mataji ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kupewa dakika cheche za kucheza.

Hata hivyo, inaelezwa dili hilo la kushangaza lina uwezekano mdogo kutokea na Palmer aliyejiunga na Chelsea mwaka 2023 kwa ada ya Pauni milioni 40,  amekuwa na kiwango bora kinachozitamanisha miamba mingi ya Ulaya kuitaka saini yake.

Vigogo wa Chelsea wanaamini wakitaka kumuuza nyota huyo wa England watamuuza mara tatu ya bei waliyomnunulia iwapo timu zinazomtaka zitaweka pesa ya kutosha mezani.

Kwa upande wa Palmer mwenyewe inaelezwa amekuwa na tetesi hana raha Stanford Bridge na anatamani kurejea Manchester huku Man United ikitajwa kuhusishwa naye dirisha lijalo la majira ya kiangazi.


Alisson Becker

INTER Milan inataka kumsajili kipa wa Liverpool na timu ya taifa ya Brazil, Alisson Becker, 33, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi lakini inakumbana na ushindani mkali kutoka kwa wapinzani wao wa Serie A, Juventus, ambao pia wanahitaji saini yake. Licha ya tetesi hizo, Liverpool bado haijaonyesha dalili za kuwa tayari kumuuza kipa huyo tegemeo, ambaye amekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya timu hiyo kwa miaka ya hivi karibuni. Mkataba wa Becker unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Harry Kane

BAADA ya kufanikisha kumshawishi beki wao wa kimataifa wa Ufaransa, Dayot Upamecano, 27, kusaini mkataba mpya mwezi uliopita, Bayern Munich sasa imeelekeza nguvu zake kwenye mazungumzo ya kumpa mkataba mpya mshambuliaji wao nyota raia wa England, Harry Kane, 32. Taarifa zinaeleza mabingwa hao wa Bundesliga wanataka kuhakikishia Kane anasalia katika timu yao kwa muda mrefu hasa kutokana na mchango wake mkubwa aliouonyesha tangu ajiunge nao akitokea Tottenham.


Alessandro Bastoni

VIGOGO wa soka Liverpool, Arsenal na Barcelona wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya beki wa Inter Milan, Alessandro Bastoni, 26 na zinapambana kuipata saini yake dirisha lijalo. Bastoni ameendelea kuonyesha kiwango cha juu Serie A na michuano ya Ulaya, jambo lililomfanya kuwa miongoni mwa mabeki wanaowindwa zaidi Ulaya. Inaelezwa Inter haiko tayari kumwachia kwa sasa ingawa kama ikiwasilishwa ofa nono inaweza kufikiria kufanya hivyo.


Leon Goretzka

ARSENAL inaongoza vita ya kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka, 31, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika dirisha lijalo majira ya kiangazi. Taarifa zinaeleza Goretzka ana nia kubwa ya kutua England kwa sababu ni ndoto yake ya muda mrefu licha ya kuhitajika na vigogo wa Italia Inter Milan, Juventus na AC Milan. Arsenal inaaminiGoretzka katikati ya kiwanja vitawapa faida kubwa msimu ujao, huku ikizingatiwa itampata bure.



Marcus Rashford

BARCELONA ipo tayari kulipa ada inayotakiwa na Manchester United ili kumsainisha mkataba wa moja kwa moja, Marcus Rashford, 28. Taarifa zinaeleza mabingwa hao wa Hispania wameridhishwa na mchango wa Rashford tangu ajiunge nao kwa mkopo na wako tayari kukamilisha dili lake dirisha la usajili wa majira ya kiangazi litakapofunguliwa. Kwa upande wa Man United, ipo tayari kumuuza staa huyo ikiwa kiasi inachohitaji kitatolewa.


Felix Nmecha

MANCHESTER City bado inaonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Felix Nmecha, 25, dirisha lijalo usajili. Nmecha ni zao la akademi ya Manchester City, lakini aliachwa miaka mitano iliyopita bila kucheza hata mechi moja ya Ligi Kuu England. Taarifa zinaeleza Kocha Pep Guardiola anamfahamu vyema mshambuliaji huyo na anaamini amekomaa kwa sasa.


Nico Schlotterbeck

REAL Madrid inaonekana kuwa katika nafasi nzuri kumsajili beki wa kimataifa wa Ujerumani, Nico Schlotterbeck, 26, anayeichezea Borussia Dortmund. Hata hivyo, Barcelona wako vitani wakihitaji saini yake, jambo lililozua ushindani mkubwa ingawa Madrid inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili. Dortmund inadaiwa kuhitaji takribani Euro 50 milioni kwa ajili ya kumuuza Schlotterbeck.