Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Amorim, mastaa Man United wapishana sehemu

Amorim Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo Mreno amewaambia mastaa wa Man United kushindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufanya vibaya Ligi Kuu England ni sehemu ya chanzo cha kufanya wafanyakazi wengine kupoteza ajira zao.

MANCHESTER, ENGLAND: MASUPASTAA wa Manchester United wameripotiwa kuvurugwa na kocha Ruben Amorim baada ya kuwashushia lawama viwango vyao vibovu uwanjani vimefanya wafanyakazi wengine wa klabu hiyo kupunguzwa kazini.

Kocha huyo Mreno amewaambia mastaa wa Man United kushindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufanya vibaya Ligi Kuu England ni sehemu ya chanzo cha kufanya wafanyakazi wengine kupoteza ajira zao.

Lakini, madai yake hayo yamedaiwa kuwakasirisha baadhi ya mastaa wanaoamini anafahamu kila kitu hali ya kifedha ya klabu hiyo tangu alipojiunga nayo katikati ya msimu.

Maneno yake yamedaiwa kuwafanya wachezaji na kocha wao kutokuwa na uhusiano wa karibuni kwa kipindi hiki ambacho mastaa hao wanapambana kuweza kufiti kwenye mtindo wa uchezaji wa Mreno huyo.

Chanzo kilifichua: “Kama ukienda Carrington utadhani wachezaji na Amorim wanaelewana vizuri sana. Lakini, ukweli wachezaji wamekasirishwa na lawama zinazoelekezwa kwao kutokana na matatizo ya kifedha ya klabu.

“Hata hivyo, hawawezi kusema chochote kuhusu kocha wao kwa sababu bado hawajazoeana vizuri. Amorim ameweka wazi anachohitaji kutoka kwao uwanjani na wao wanapambana kumpa.

“Lakini, wakati baadhi wakimsapoti kwenye mtindo wake, kinachoelezwa, bado wachezaji hawana uhuru wa kutoa maoni yao kwa kile anachotaka Amorim. Wanafanya wanachoambiwa wafanye, iwe ni kizuri au kibaya...wachezaji hao wawilivyo hawataki kumwonyesha kocha ishara yoyote hawafurahii la italeta matatizo."

Chanzo hicho kilifichua Amad Diallo na Amorim wamekuwa na muunganiko mzuri, huku nahodha wa timu hiyo, Bruno Fernandes akitumika kama kiungo muhimu katika kumuunganisha kocha na wachezaji wengine.

Baada ya mechi ya ushindi wa mabao 3-2 kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Ipswich Town, Jumatano iliyopita, kiungo Fernandes alisema falsafa za kocha Amorim bado hazijaanza kuleta matunda kama inavyohitajika.