Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa azichanganya Liverpool, Chelsea

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 ameonyesha kiwango kikubwa sana katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya kujiunga na Sunderland kwa dau la Pauni 9 milioni akitokea NEC Nijmegen.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA na Liverpool zinadaiwa kuwa katika vita kali ya kuiwania saini ya kipa  wa Sunderland, Robin Roefs dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 ameonyesha kiwango kikubwa sana katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya kujiunga na Sunderland kwa dau la Pauni 9 milioni akitokea NEC Nijmegen.

Kwa sasa kipa huyo wa timu ya taifa ya vijana ya Uholanzi chini ya miaka 21, ambaye pia tayari amepewa nafasi kikosi cha wakubwa na kocha Ronald Koeman, anatajwa kuwa na thamani ya takribani Pauni 50 milioni.

CHEL 01

Hata hivyo, kiwango hicho cha fedha hakijazizuia Chelsea na Liverpool ambazo zote zinatafuta makipa dirisha lijalo.

Chelsea inatafuta kipa mwingine kwa sababu hairidhishwi na kiwango cha Roberto Sanchez, huku Liverpool ikitaka kusajili kwa sababu  Alisson anataka kuondoka mwisho wa msimu kwenda kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine na Juventus inatajwa kuwa moja ya klabu zinazomhitaji.

Kipa namba mbili wa Liverpool, Giorgi Mamardashvili, bado hajaonyesha uwezo wa kuaminika wa kurithi nafasi ya nyota huyo wa Brazil kwa muda mrefu.

Roefs amekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Sunderland kubaki salama Ligi Kuu England baada ya kupanda msimu huu.

CHEL 02

Ikiwa Sunderland itakubali kumuuza, itanufaika kwa faida kubwa kutokana na kiasi kidogo ambacho ililipa ili kumnunua fundi huyo.

Msimu huu, Roefs tayari amecheza mechi 10 kati ya  33 za Ligi Kuu England bila ya kuruhusu bao, akiisaidia Sunderland kushika nafasi ya 12 kwenye msimamo, nafasi moja juu ya mahasimu wao wakubwa Newcastle United.