Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinda Arsenal aingia anga za Madrid

Muktasari:

  • Myles ameonyesha kiwango bora sana chini ya  Mikel Arteta kwa msimu huu ambapo amecheza mechi  39, akifunga bao moja na kutoa asisti tatu.

MADRID, HISPANIA: MABOSI wa Real Madrid wametua kwa beki wa kushoto wa Arsenal Myles Lewis-Skelly na wanataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Myles ameonyesha kiwango bora sana chini ya  Mikel Arteta kwa msimu huu ambapo amecheza mechi  39, akifunga bao moja na kutoa asisti tatu.

Hata hivyo, licha ya kusaini mkataba wake wa kwanza kama mchezaji wa kulipwa  Oktoba 2023, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 anaweza tayari kuondoka Kaskazini mwa London na kumaliza ushirikiano wa miaka kumi na klabu hiyo katika dirisha lijalo.

Hii ni kwa sababu mkataba wake umebakisha mwaka mmoja tu na, Real Madrid wameshaanza kuchunguza hali yake.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Guardian, mazungumzo kati ya mchezaji na Arsenal kuhusu mkataba mpya "hayendi vizuri."

Hii imemfanya Madrid kuwa katika tahadhari kubwa ya kumsajili mlinzi huyo wa kushoto wa timu ya taifa ya England.

Madrid hadi sasa tayari imemsajili beki wa kushoto wa timu ya taifa ya England kutoka Liverpool, Trent Alexander-Arnold, kwa ada ya Pauni 10 milioni na ina matumaini ya kupata staa mwingine kutoka nchi hiyo.

Kwa mjumuisho wa Jude Bellingham aliyeko tayari kwenye timu, Madrid inaweza kuwa na nyota watatu wa England ikiwa itafanikisha dili hili la Myles.

Madrid imevutiwa sana na staa huyu kwa sababu ana uwezo wa kucheza shemu mbalimbali kiwanjani mbali ya beki wa kushoto, anaweza kucheza kama kiungo namba sita au nane