Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jota ni balaa lingine Liverpool

Jota ni balaa lingine Liverpool

Muktasari:

  • HUENDA tukaona ule utatu wa Liverpool, Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino ukipotea kutokana na uwepo wa Diogo Jota.

HUENDA tukaona ule utatu wa Liverpool, Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino ukipotea kutokana na uwepo wa Diogo Jota.

Wengi walikuwa wakimpa muda pengine ule moto ambao alianza nao tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Wolves, ungepotea, lakini imekuwa tofauti anachofanya ni kufunga tu, kitu ambacho hata kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, anakifurahia.

Ni wazi Jota anampasua kichwa Klopp kwenye upangaji wa kikosi chake cha kwanza nani aanze na nani asubiri kati ya wale washambuliaji wake watatu ambao wamekuwa wakianza kwa pamoja kwenye michezo mbalimbali.

Mreno huyo ni mzuri akisimama kama mshambuliaji wa mwisho lakini pia anaweza kutokea pembeni, uamuzi ni wa Klopp juu ya namna ya kumtumia, uwezo wake unanifanya kuamini kuwa anaweza kuiadhibu Aston Villa wikiendi ijayo.

Rekodi yake inaonyeshwa kuwa ameifungia Liverpool mabao manane kwenye michezo 13 aliyochezea ya Ligi Kuu England.