Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jesus ni mwendo wa kusoma Biblia tu

Muktasari:

  • Lakini, kwenye hilo hakuna mashaka pia Arsenal ilihitaji huduma yake kwa muda wote aliokuwa nje ya uwanja, huku Mbrazili huyo akiwa fiti katika kipindi mwafaka cha mechi nyingi za Krismasi.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Arsenal, Gabriel Jesus amefichua amekuwa kwenye mashaka makubwa kwa miezi 11 iliyopita.

Lakini, kwenye hilo hakuna mashaka pia Arsenal ilihitaji huduma yake kwa muda wote aliokuwa nje ya uwanja, huku Mbrazili huyo akiwa fiti katika kipindi mwafaka cha mechi nyingi za Krismasi.

Alirejea uwanjani Jumatano iliyopita kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Arsenal iliposhinda 3-0 dhidi ya Club Bruges baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu alipoumia goti katika mechi dhidi ya Manchester United, Januari mwaka huu. Na sasa amerudi kwenye mpango wa kuhakikisha Arsenal inafanya kweli na kubeba mataji msimu huu.

Jesus alinaswa na Arsenal kwa ada ya Pauni 45 milioni akitokea Manchester City mwaka 2022, lakini kurejea kwake kikosini kunaweza kuwa habari mbaya kwa straika Viktor Gyokeres, ambaye amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya misuli na kushindwa kufanya mambo ya maana katika kikosi cha Arsenal katika kutimiza ndoto za kushinda taji la Ligi Kuu England.

Jesus amesema: “Swali la kwanza ambalo nimekuwa nikijiuliza ni hili, kwa nini? Kila siku, wiki mbili au tatu za mwaka baada ya kurejea uwanjani nikitokea kwenye majeraha, nimekuwa nikijiuliza nini kimenikuta. Baada ya hapo, naelewa namhitaji Yesu, namhitaji Mungu na nimekuwa nikisoma Biblia.”

Jesus aliishia tu kukaa benchini kwenye mechi dhidi ya Brentford na Chelsea kabla ya kuingia dakika 62 kumbadili Gyokeres katika mechi dhidi ya Bruges. Alionekana kuwa kwneye hali nzuri, akipiga pasi sahihi 14 ukinganisha na tano tu za Gyokeres. Jesus alifunga mabao 26 katika mechi 97 alizochezea Arsenal na sasa kurudi kwake uwanjani kutamfanya Kocha Mikel Arteta kuwa na machaguo mengi ya kutosha kwenye safu yake ya ushambuliaji.