Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamie Redknapp amkingia kifua Slot, aomba mashabiki wamvumilie

REDNAPP Pict

Muktasari:

  • Liverpool ambayo ni bingwa mtetezi wa EPL imepoteza mechi sita kati ya saba za mwisho, ikiwemo kichapo cha jana Jumamosi cha 3-0 kutoka kwa  Nottingham Forest kwenye Uwanja wa Anfield na kiwango cha uchezaji kimeibua maswali mengi.

Mchambuzi wa soka wa England, Jamie Redknapp, amewataka mashabiki wa Liverpool kumvumilia kocha Arne Slot, ambaye anapitia kipindi kigumu kwa sasa, kufuatia kikosi hicho kushindwa kuonyesha uwezo na kupata matokeo mazuri uwanjani.

Liverpool ambayo ni bingwa mtetezi wa EPL imepoteza mechi sita kati ya saba za mwisho, ikiwemo kichapo cha jana Jumamosi cha 3-0 kutoka kwa  Nottingham Forest kwenye Uwanja wa Anfield na kiwango cha uchezaji kimeibua maswali mengi.

Hata hivyo, kwa kuwa Slot aliiongoza Liverpool kutwaa taji msimu uliopita kabla ya msimu kuisha, bado ana akiba ya imani na heshima miongoni mwa mashabiki, jambo ambalo Redknapp amelisisitiza.

Akizungumza kupitia Sky Sports, Redknapp ambaye alicheza soka akiwa na klabu za AFC Bournemouth, Liverpool FC Tottenham Hotspur na Southampton amesema: “Lazima uwe mvumilivu kwa sasa. Arne Slot anastahili hilo baada ya alichokifanya mwaka jana, na watarudi. Huu unaweza kuwa msimu ambao utakuwa na mambo ya kupanda na kushuka sana.”

RED 01

Mchambuzi huyo pia amebainisha kwamba, msiba wa kumpoteza Diogo Jota na ugumu wa baadhi ya wachezaji wapya kuzoea maisha ya Anfield vimechangia changamoto kwa kocha huyo raia wa Uholanzi.

Kichapo cha Forest kilikuwa kigumu zaidi ukizingatia kuwa ni miezi 14 tangu Forest ipate ushindi wake wa mwisho katika Uwanja wa Anfield. Msimu uliopita, huo ndio ilikuwa mechi pekee wa ligi ambao Liverpool walipoteza nyumbani, lakini msimu huu tayari wameshapoteza miwili, ikiwemo dhidi ya Manchester United.

Liverpool pia imefungwa na Chelsea, Manchester City, Crystal Palace, Brentford, na Galatasaray tangu mfululizo wao wa ushindi ulipokatika mwishoni mwa Septemba.

Katika mechi hiyo, Slot hakuwa na Florian Wirtz na Conor Bradley ambao ni majeruhi kwa sasa, huku Jeremie Frimpong akiwa bado nje. Hali hiyo ilimlazimu kumtumia Curtis Jones kama beki wa kulia. Alexander Isak alirejeshwa kama mshambuliaji wa kati, huku Cody Gakpo akirudi upande wa kushoto na hivyo kumfanya Hugo Ekitike kuanzia benchi.

RED 02

Isak alianza mchezo akicheza hadi dakika ya 68 kabla ya kutolewa, huku Ekitike akiingia muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza.

Akizungumza na Match of the Day ya BBC baada ya mechi hiyo, Slot alisema: “Ni kukatishwa tamaa tena. Tulianza vizuri kwa dakika 30 za mwanzo. Tuliporuhusu bao la kwanza, hatukuweza kucheza kama tulivyocheza mwanzoni.”

Kuhusu kufungwa ndani ya dakika 60 za kipindi cha pili, Slot aliongeza: “Bila shaka ilikuwa pigo. Tayari ilikuwa ngumu kuwa nyuma 1-0 dhidi ya timu inayojilinda kwa kila kitu. Ni rahisi hivyo.”

Alimalizia kwa kusema: “Katika siku chache, tunacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya tena, kisha mechi tatu za EPL kwa muda mfupi. Inabidi kupambana katika Uwanja wa mazoezi ili kufanya kazi kwa bidii sana. Tunajaribu kila siku kufanya hivyo. Ni muhimu kuwa na wachezaji wenye uzoefu na ubora, lakini kwa sasa mambo hayaendi.”