Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamie Carragher: Slot, piga chini Mo Salah

JAMIE Pict

Muktasari:

  • Mo Salah, ambaye alikuwa kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, mambo yamekuwa magumu msimu huu, akiwa amefunga mara nne tu katika mechi 11.

LIVERPOOL, ENGLAND: STAA wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amemwambia kocha wa miamba hiyo ya Anfield, Arne Slot anapaswa kumpiga chini Mohamed Salah endapo staa huyo wa Misri ataendelea kufanya hovyo uwanjani.

Mo Salah, ambaye alikuwa kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, mambo yamekuwa magumu msimu huu, akiwa amefunga mara nne tu katika mechi 11.

Na kwenye mechi zote hizo 11 alianzishwa na amecheza kwa dakika zote 90 mara nyingi.

Na kwenye mechi za Liverpool katika mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ameanzishwa kwenye mechi mbili tu kati ya nne na alifunga bao dhidi ya Atletico Madrid, alitoka patupu kwenye mechi dhidi ya wapinzani wa kweli kwenye michuano hiyo, Real Madrid.

Mo Salah anajiandaa kukosekana kwenye mechi za Liverpool zitakazochezwa kati ya Desemba mwishoni na Januari, kwa kuwa atakwenda kujiunga na timu yake ya taifa ya Misri itakayokuwa na majukumu kwenye michuano ya Afcon huko Morocco.

JAMI 01

Na sasa kocha Slot anapaswa kutafuta namna ya kucheza bila ya huduma ya mshambuliaji wake huyo kwa kipindi ambacho hatakuwapo, lakini Carragher anaamini sasa ni wakati wa kumweka kando Mo Salah kwa sababu kiwango chake uwanjani kimeshuka.

“Kama mbele mabao hayafungwi na huku nyuma yanaruhusiwa yaingie kwenye nyavuni hiyo ina maana kimbinu mambo yamekwamba na ni hatari kuendelea kumruhusu Mo Salah aendelee kuwapo pale mbele,” amesema Carragher.

“Hivyo ni mawili, ama arudi nyuma kusaidia ulinzi, au achezeshwe mtu mwingine. Na ndio maana nilishasema hili wiki chache zilizopita kuhusu Mo Salah kuendelea kuanza kila wiki hasa kwenye mechi za ugenini, hili linapaswa kukoma.”

Mchambuzi mwenzake, Wayne Rooney naye alikuwa na kitu cha kuzungumza huku akidai wapinzani wa Liverpool wamekuwa wakiiandama timu hiyo kupitia kwenye upande wa kulia kwa sababu wanafahamu wazi Mo Salah harudi nyuma kukaba, hivyo jambo hilo linawafanya mabeki Conor Bradley, Jeremie Frimpong au yeyote atakayepangwa kuwa kwenye wakati mgumu.

JAMI 02

“Ni lazima itafutwe namna ya kumrudisha kwenye ubora wake au kukaribia ubora wake. Lakini, hii ya kumchezesha, kumchezesha tu, haisaidii kitu.”

Liverpool itarudi mzigoni baada ya mechi mapumziko ya mechi za kimataifa kumenyana na Nottingham Forest, Novemba 22 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Kisha itakipiga na PSV Eindhoven kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na baada ya hapo mechi itakayofuatia itakipiga na West Ham United.

Mo Salah kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Misri kwa ajili ya michezo ya Al-Ain International Cup. Michuano hiyo ya kirafiki itaishuhudiwa Misri ikikabiliana na timu za Cape Verde, Iran na Uzbekistan katika mapumziko ya ligi kupisha kalenda ya FIFA.