Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ian Wright ampa mtihani Mikel Arteta

WRIGHT Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo liliwafanya wachambuzi wenzake, Jamie Redknapp na Micah Richards, kumtania kwa kudai amefanya kama mpishi maarufu 'Salt Bae' ambaye alikosolewa huko nyuma kwa kuingia uwanjani kushangilia na wachezaji.

ARSENAL imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya England 2025-2026 baada ya kusubiri kwa miaka 22, huku sherehe za ubingwa huo zikitawaliwa na matukio ya kihistoria na ya kufurahisha katika uwanja wa Selhurst Park. 

Katika sherehe hizo, mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Ian Wright, alijikuta katikati ya matukio hayo baada ya kuvishwa medali ya ushindi na mchezaji Gabriel Martinelli wakati akiwa kwenye majukumu yake ya uchambuzi wa soka na kituo cha Sky Sports, huku gwiji huyo akimpa Kocha Mikel Arteta mtihani mwingine.

WR 02

Tukio hilo liliwafanya wachambuzi wenzake, Jamie Redknapp na Micah Richards, kumtania kwa kudai amefanya kama mpishi maarufu 'Salt Bae' ambaye alikosolewa huko nyuma kwa kuingia uwanjani kushangilia na wachezaji.

Wright (62) alionyesha hisia za furaha na kusisitiza kuwa ubingwa huo ni jibu tosha kwa dhihaka na ukosoaji ambao mashabiki na timu ya Arsenal wamekuwa wakipokea kwa miaka minne mfululizo. 

WR 01

Ameeleza kuwa, mbinu zote na mifumo ya kocha Mikel Arteta, ambazo zamani zilionekana kama vitu vya mzaha, hatimaye imelipa na kuifikisha timu hiyo kwenye kilele cha mafanikio. 

Akiwa na medali hiyo shingoni, Wright alijumuika na wachezaji pamoja na wafanyakazi wa Arsenal kusherehekea taji hilo ambalo limezima kelele zote za wapinzani wao.

WR 03

Kufuatia mafanikio hayo, Wright ametoa kauli nzito akidai kuwa Mikel Arteta yuko hatua moja tu ya kuwa kocha bora zaidi katika historia ya Arsenal, akimzidi hata kocha nguli, Arsene Wenger. 

Wright amekiri mchango mkubwa wa Wenger katika kujenga uwanja mpya wa Emirates na kuifikisha timu hiyo Ligi ya Mabingwa Ulaya mara kwa mara, lakini akabainisha kuwa Wenger hakuwahi kubeba taji hilo la Ulaya.

Amehitimisha kwa kusema ikiwa Arteta atafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ataweka rekodi ambayo hakuna kocha mwingine yeyote wa Arsenal amewahi kuifikia, hivyo kuwa kocha mkuu bora zaidi wa muda wote klabuni hapo.