Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hugo Broos atetea uamuzi wa kuwaita Mofokeng, Mokwana

BROOS Pict

Muktasari:

  • Mofokeng na Mokwana walikosa mechi kadhaa za hivi karibuni za timu ya taifa kwa sababu tofauti, lakini Broos aliyelitangaza kikosi hicho jana Jumatatu, Desemba 1, 2025 amesema kiwango kizuri walichoonyesha wachezaji hao katika klabu zao kimekuwa sababu ya kuwapa nafasi katika kikosi chake cha wachezaji 25.

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana, Hugo Broos, amewapongeza Relebohile Mofokeng na Elias Mokwana, akisema wana uwezo wa kufanya vizuri katika fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), baada ya kuwajumuisha kwenye kikosi cha mwisho kitakachoshiriki mashindano hayo nchini Morocco.

Mofokeng na Mokwana walikosa mechi kadhaa za hivi karibuni za timu ya taifa kwa sababu tofauti, lakini Broos aliyelitangaza kikosi hicho jana Jumatatu, Desemba 1, 2025 amesema kiwango kizuri walichoonyesha wachezaji hao katika klabu zao kimekuwa sababu ya kuwapa nafasi katika kikosi chake cha wachezaji 25.

Mofokeng, aliyekosa mechi tano zilizopita za Bafana Bafana, amekuwa kwenye kiwango bora akiisaidia Orlando Pirates katika mechi zao nne zilizopita, akiibuka mchezaji bora wa mechi wakati wa ushindi wa 2-0 dhidi ya Durban City, kwenye Uwanja wa Moses Mabhida mwishoni mwa wiki iliyopita.

BROO 01

“Kuhusu Relebohile Mofokeng, unajua ninampenda kwa sababu ni mchezaji mwenye kipaji. Alikuwa na matatizo kadhaa miezi michache iliyopita kutokana na majeraha, na nilifurahi kumuona amerudi uwanjani hivi karibuni akiichezea Pirates. Kwa hiyo sikuwa na shaka hata kidogo kumchagua.” Broos amesema.

Mokwana pia alikosa mechi za Bafana Bafana miezi iliyopita baada ya kuondoka Esperance ya Tunisia na kujiunga na klabu ya Al-Hazem ya Saudi Pro League, ambako amekuwa kwenye kiwango bora katika wiki za karibuni.

“Yuko kwenye hali nzuri, na unajua napenda winga ambao wana kasi na uwezo wa kupita, na Elias ni aina hiyo ya mchezaji. Ni muhimu kujua kwamba tunawategemea.” Broos amesema.

BROO 03

Broos amesema nafasi ya Mokwana imeimarika zaidi kutokana na Al-Hazem kutumika kama mshambuliaji wa kati, jambo analoamini linaweza kuisaidia Bafana Bafana, kwenye kampeni za kuwania ubingwa wa AFCON 2025 nchini Morocco.

“Katika miezi ya karibuni tumetazama mechi zake kadhaa huko Al-Hazem, na amekuwa akicheza vizuri ingawa hawamchezeshi katika nafasi yake ya asili. Wanamchezesha kama mshambuliaji wa kati, na hii inamaanisha tunaweza kumchezesha hapo ikiwa tutamuhitaji.”

Broos pia ametangaza wachezaji waliowekwa ‘standby’ kama beki Thabo Moloisane, kiungo Mduduzi Shabalala, na mshambuliaji Iqraam Rayners. Akieleza kwa nini watabaki.

“Tutawaomba wabaki hapa, waendelee kujifua na kudumisha utimamu ili ikitokea jambo lolote wawe tayari. Sitaki kuwachukua kwenye mashindano kwa sababu mazoezini nitakuwa na wachezaji 28 kila siku, na hilo si rahisi kufanya kazi.

“Tuombe tusihitaji huduma yao kwa sasa, kwa sababu tukiwahitaji itakuwa maana yake kuna tatizo. Lakini pia natumaini kutakuwepo nafasi kwao kutufuata Morocco, pale itakapohitajika,” amesema

BROO 02

Mabadiliko makubwa pekee kwenye kikosi cha Broos ni ujumuishwaji wa beki mchanga Tylon Smith, aliyekuwa mchezaji bora wa mashindano ya U-20 AFCON mwaka huu, na winga Shandre Campbell. 

Broos amesema wawili hao wamechaguliwa kwa ajili ya maendeleo ya baadaye, lakini wameitwa kama wachezaji wenye vipaji vinavyoibuka kwa matumizi ya dharura nchini Morocco.

“Hao ni wachezaji wenye kipaji, Tylon alicheza Afcon ya U-20 na Kombe la Dunia, na ni jambo la kushangaza kuwa Club Brugge hawakutaka kumruhusu Shandre Campbell kucheza Kombe la Dunia la U-20. Hii ni nafasi nzuri kwao kuzoea wakiwa na timu ya taifa ya wakubwa na kuona kinachoendelea kwenye mazoezi ya Bafana, na wana mengi ya kujifunza katika wiki zijazo.

“Nimewaita kwa sababu ya ubora wao, lakini hatutarajii kama watacheza mechi za AFCON 2025. Ikitokea nafasi watacheza, lakini muhimu zaidi kwao ni kupata uzoefu wa kuwa sehemu ya Bafana Bafana katika kiwango cha juu,” amesema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Katika fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), Bafana Bafana imepangwa Kundi B sambamba na Misri, Angola, pamoja na Zimbabwe.

Bafana Bafana itaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa AFCON 2025, Desemba 22 kwa kucheza dhidi ya Angola, kisha itaikabili Misri Desemba 26 na katika mechi ya mwisho itakutana na Zimbabwe Desemba 29.