Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Howe afunguka kitu kuhusu Isak

Muktasari:

  • Newcastle, ambayo inamthaminisha straika huyo kuwa na thamani ya Pauni 150 milioni imemwengua kwenye mazoezi ya wenzake baada ya Liverpool kuhitaji huduma yake dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

NEWCASTLE, ENGLAND: KOCHA wa Newcastle United, Eddie Howe amekiri kama ingekuwa rahisi kumshawishi straika Alexander Isak abaki kwenye kikosi chake angefanya hivyo muda mrefu sana.

Newcastle, ambayo inamthaminisha straika huyo kuwa na thamani ya Pauni 150 milioni imemwengua kwenye mazoezi ya wenzake baada ya Liverpool kuhitaji huduma yake dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Na baada ya mechi ya Jumamosi ya kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Atletico Madrid, kocha Howe alisema: “Klabu itafanya uamuzi juu ya hatima yake na mimi sifahamu utakuwa uamuzi gani.

“Sawa, nitapenda kitakachotokea, lakini nataka wachezaji wanaotaka kubaki na kucheza soka kwenye klabu hii. Kama ingekuwa rahisi kumshawishi, ningefanya hivyo muda mrefu.”

Kipigo hicho kutoka kwa Atletico kwenye mechi ya kirafiki hiyo ina maana, Newcastle itakwenda kumenyana na Aston Villa kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England bila ya kushinda mchezo wowote katika pre-season.

Howe alikiri kikosi chake kimekuwa hakina makali kwenye goli la wapinzani baada ya kumkosa Isak, lakini aliongeza: “Huo unaweza kuwa uchambuzi wa jumla, lakini bado tunashinda mechi.”

Katika hatua nyingine, kocha Howe aligoma kukubali mabosi wa Newcastle wanaweza wakafuta mpango wa kumuuza Isak kwenda Liverpool, baada ya kushuhudia ofa yao ya kwanza ya Pauni 110 milioni ikigomewa.