Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hojlund Napoli, Osimhen Man United

HOJLUND Pict

Muktasari:

  • Hojlund, 22, amekuwa akihusishwa sana na mpango wa kuachana na miamba ya Old Trafford kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA wa Manchester United, Rasmus Hojlund amewekwa kwenye rada ya Napoli na huenda dili lake likamhusisha straika wa Kinigeria, Victor Osimhen, imeelezwa.

Hojlund, 22, amekuwa akihusishwa sana na mpango wa kuachana na miamba ya Old Trafford kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Akiwa amefunga mabao manane tu katika mechi 39 alizochezea Man United msimu huu, straika huyo ameshindwa kumshawishi kocha mpya Ruben Amorim na mabosi wa timu hiyo.

Amewekwa kwenye orodha ya kikosi kilichorithiwa na kocha Amorim, wachezaji ambao bosi wa timu bilionea, Sir Jim Ratcliffe alisema hawana viwango vya kutosha kuwa Man United.

Wakati bosi huyo mpya akiwaza kuijenga upya Man United, straika Hojlund, aliyesajiliwa kwa Pauni 72 milioni, anaweza kuachwa kwa pesa kidogo sana.

Na gazeti la La Gazzetta dello Sport la Italia linafichua kwamba Napoli inahitaji huduma ya straika huyo. Man United inahitaji Pauni 50 milioni kwenye mauzo ya mshambuliaji huyo, ambaye mwenyewe ameweka wazi milango ya kurudi Italia.

Napoli inaamini kumshawishi Hojlund kurudi Italia hakitakuwa kitu kigumu na sasa mpango wa kubadilishana wachezaji unaweza kufanyika, ambapo Osimhen anaweza kutimkia Old Trafford kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Osimhen, 26, kwa sasa anacheza kwa mkopo Galatasaray amekuwa akihusishwa na mpango wa kutimkia kwenye Ligi Kuu England mwisho wa msimu huu.

Atarudi Naples mwisho wa msimu, lakini kuna uwezekano mkubwa akauzwa kabla ya msimu wa 2025-26 haujaanza. Na kinachoripotiwa ni kwamba Osimhen yupo kwenye orodha ya mastraika watano waliopo kwenye rada ya Man United kwa ajili ya dirisha lijalo.

Mwandishi wa habari wa masuala ya usajili, Alex Crook alisema: "Nadhani (Victor) Osimhen atahusika zaidi kwa sababu ni aina ya mchezaji ambaye Man United wanaweza kummudu. Nadhani mahitaji yake ya mshahara haitakuwa shida Man United. Kwenye hilo sitashangaa pia kama Hojlund atarudi Italia, Napoli wanamtaka na Osimhen anatakiwa kule kwingine."

Osimhen amefunga mabao 26 na asisti tano kwenye mechi 30 alizocheza msimu huu kwenye kikosi cha Galatasaray ya Uturuki.