Hizi hapa Gemu za uwekezaji Ulaya
Muktasari:
- Kwenye Bundesliga, Borussia Monchengladbach itakipiga na Augsburg, wakati Bayer Leverkusen itakuwa ugenini kucheza na Holstein Kiel, huku Mainz 05 ikimalizana na St. Paul, Wolfsburg na VfL Bochum na Borussia Dortmund itacheza na Union Berlin kwa mechi za Jumamosi, wakati Jumapili, RB Leipzig itacheza na FC Heidenheim, Bayern Munich na Eintracht Frankfurt, wakati Hoffenheim itakipiga na VfB Stuttgart.
MUNICH, UJERUMANI: MAMBO ni moto kwa vijana wawekezaji kwenye soka la Ulaya wikiendi hii, kutokana na kupigwa mechi matata kabisa katika mikikimikiki ya Ligi Kuu.
Kwenye Bundesliga, Borussia Monchengladbach itakipiga na Augsburg, wakati Bayer Leverkusen itakuwa ugenini kucheza na Holstein Kiel, huku Mainz 05 ikimalizana na St. Paul, Wolfsburg na VfL Bochum na Borussia Dortmund itacheza na Union Berlin kwa mechi za Jumamosi, wakati Jumapili, RB Leipzig itacheza na FC Heidenheim, Bayern Munich na Eintracht Frankfurt, wakati Hoffenheim itakipiga na VfB Stuttgart.
Kwenye La Liga, kazi inaanza Jumamosi, ambapo Alaves itakuwa nyumbani kucheza na Espanyol, Rayo Vallecano na Villarreal, wakati Valencia itakuwa na kazi mbele ya Atletico Madrid na Las Palmas ipo nyumbani kucheza na Barcelona. Jumapili shughuli itakuwa baina ya Athletico Bilbao na Real Vallladolid, Real Madrid na Girona, Getafe na Real Betis na Real Sociedad itaonyeshana ubabe na Leganes.
Huko kwenye Serie A, zitapigwa mechi nne Jumamosi, ambapo Parma itakuwa nyumbani kukipiga na Bologna, Venezia itacheza na Lazio, Torino na AC Milan, wakati wababe Inter Milan watamaliza na Genoa. Jumapili ni kasheshe, Como 1907 itacheza na Napoli, Hellas Verona itakipiga na Fiorentina, wakati Empoli itamaliza utata na Atalanta na Juventus itaifuata Cagliari.
Balaa la Ligue 1, litakuwa huko Lille itakapocheza na AS Monaco, kabla ya Saint-Etienne kukipiga na Angers na Auxere kucheza na Marseille katika vipute vya Jumamosi. Jumapili, Nantes itacheza na Lens, Le Havre na Toulouse, wakati Nice itamaliza ubishi na Montpellier, Strasbourg na Brest na Lyon itakuwa na kasheshe mbele ya Paris Saint-Germain.