Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hivi ndivyo mziki wa Trent Madrid utakavyokuwa

Muktasari:

  • Trent anazifikisha mwisho zama zake kwenye kikosi cha Liverpool baada ya kunyakua mataji mawili ya Ligi Kuu England, Kombe la FA, Kombe la Ligi mara mbili, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Dunia la Klabu.

LIVERPOOL,  ENGLAND: BEKI wa kulia, Mwingereza Trent Alexander-Arnold ametangaza ataachana na Liverpool mwishoni mwa msimu.

Trent anazifikisha mwisho zama zake kwenye kikosi cha Liverpool baada ya kunyakua mataji mawili ya Ligi Kuu England, Kombe la FA, Kombe la Ligi mara mbili, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Dunia la Klabu.

Beki huyo ambaye ni mzaliwa wa Liverpool, Alexander-Arnold, 26, amekuwa kwenye kikosi hicho cha Anfield tangu alipokuwa na umri wa miaka sita na kuwa mmoja wa wachezaji mahiri kabisa walioibukia kutoka kwenye akademia ya klabu hiyo tangu alipoanza kucheza mechi yake ya kwanza 2016, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18.

Lakini, baada ya kucheza mechi zaidi ya 350 kwenye kikosi cha Liverpool sasa ataenda Hispania kwenye hatua inayofuata na maisha yake ya soka. Kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na Real Madrid na kinachoripotiwa amesaini mkataba wa miaka mitano kwenye kikosi hicho cha La Liga, akilipwa mshahara wa Pauni 240,000 kwa wiki, pamoja na mkwanja wa kutosha wa ada ya kusaini.

Kumekuwa na taarifa kutoka Hispania, ofa iliyowekwa mezani huko Real Madrid ni mkataba wa miaka sita.

Mashabiki wa Liverpool walikuwa wakisubiri hatima ya Alexander-Arnold baada ya mastaa wengine, Mohamed Salah na Virgil van Dijk kusaini dili mpya za kuendelea kubaki Merseyside. Na sasa Alexander-Arnold alithibitisha mwenyewe kwa mashabiki anaondoka baada ya kutoa ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wiki moja baada ya Liverpool kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England.

Taarifa yake ilisomeka hivi: “Baada ya miaka 20 hapa Liverpool Football Club, sasa ni muda wa kuthibitisha kwamba naondoka mwishoni mwa msimu. Huu ni uamuzi mgumu ambao nimewahi kufanya kwenye maisha yangu. Wengi walishangaa kwanini sikusema hili mapema, lakini malengo yangu nilikuwa nimeeleza kwenye mafanikio ya timu, kushinda taji la 20. Hii ni klabu niliyokuwa hapa kwa miaka yangu yote, miaka yangu yote 20. Mapenzi yangu kwa timu hii hayatakufa.”

Na taarifa ya Liverpool ilisomeka: “Trent Alexander-Arnold ameiambia Liverpool FC dhamira yake ya kuondoka mwishoni mwa msimu wakati mkataba wake utakapofika ukomo. Mchezaji huyo wa miaka 26 atafikisha mwisho miongo yake miwili mwishoni mwa msimu huu na ataondoka Anfield mkataba wake utakapofika mwisho Juni 30, 2025.”

Licha ya kwamba bado hakuna tangazo rasmi, kinachoonekana Real Madrid anakwenda  kuungana na swahiba wake na Mwingereza mwenzake, Jude Bellingham.

Madrid ilifanya jaribio la kumsajili Alexander-Arnold dirisha la Januari ili kwenda kuchukua nafasi ya beki wa kulia Dani Carvajal, aliyekuwa majeruhi.