Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ni zaidi Sundowns, FAR Rabat kwa Wareno hao

Muktasari:

  • Mamelodi Sundowns wanaingia kwenye Uwanja wa Moulay Abdellah wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika nyumbani kwao Afrika Kusini wiki iliyopita, hali inayowalazimu wenyeji FAR Rabat kushinda nyumbani ili kurudia mafanikio yao ya mwaka 1985, walipotwaa taji hilo.

Rabat, Morocco: HATMA ya mfalme wa Ligi ya Mabingwa Afrika itajulikana leo, Jumapili nchini Morocco, lakini simulizi ya kuvutia ya mchezo huo wa marudiano inakwenda mbali zaidi ya kilichotokea Pretoria na hapo Rabat.

Mamelodi Sundowns wanaingia kwenye Uwanja wa Moulay Abdellah wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika nyumbani kwao Afrika Kusini wiki iliyopita, hali inayowalazimu wenyeji FAR Rabat kushinda nyumbani ili kurudia mafanikio yao ya mwaka 1985, walipotwaa taji hilo.

Fainali hii pia ni ishara kubwa ya kukua kwa ushawishi wa makocha wa Kireno barani Afrika, huku kocha wa Sundowns, Miguel Cardoso atakuwa na kibarua kizito mbele ndugu yake kocha wa FAR Rabat, Alexandre Santos katika kusaka taji kubwa zaidi kwa upandeklabu barani humo.

Cardoso anatafuta kujenga upya taswira yake baada ya maumivu ya fainali zilizopita. huku Santos anajaribu kuipa FAR Rabat taji lao la kwanza la Afrika ndani ya miaka 40 na kuirejesha kileleni mwa soka la Afrika.

Kocha mmoja wa Kireno pekee ndiye atakayoinua kombe leo, lakini wote wawili tayari wamethibitisha bora wao.

Soka la Afrika si tena sehemu ya mwisho kwa makocha wa kigeni. Ni sehemu ya kuthibitisha uwezo, mazingira ya presha kubwa, na kwa Cardoso na Santos, ni jukwaa kubwa la kujenga sifa zinazovuka mipaka ya bara.

Kocha Cardoso anaingia katika fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanya hivyo akiwa na Esperance de Tunis pamoja na Sundowns, tukio hili lina maana kubwa zaidi ya mafanikio binafsi. Anaamini soka la Ureno bado halijatambua kikamilifu ukubwa wa mafanikio yanayofanywa na makocha wake barani Afrika.

“Nadhani jamii ya soka ya kimataifa barani Ulaya, hasa Ureno, haielewi kiwango cha ushindani wa Ligi ya Mabingwa Afrika,”€ 

“Ni aibu kwa nchi yangu kutotambua ukubwa wa mafanikio ambayo baadhi ya makocha wa Kireno wamekuwa wakiyapata Afrika”

Kauli za Cardoso zinaonyesha uzito wa fainali ya leo, Jumapili. Makocha wawili wa Kireno wamezifikisha klabu mbili kubwa za Afrika katika fainali ya mashindano makubwa zaidi ya klabu barani, lakini wote wawili wamekiri kuwa kazi yao mara nyingi haithaminiwi nyumbani kwao kama mafanikio ya aina hiyo Ulaya.

Kocha huyo wa Sundowns alimtaja Manuel Jose, aliyekuwa mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi katika historia ya soka la klabu Afrika baada ya kushinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa akiwa na Al Ahly.

“Hata Manuel Jose hakutambuliwa kwa kiwango cha kazi aliyofanya hapa, na hiyo ni aibu kubwa,”  alisema Cardoso.

“Wanaona bora kumtambua mtu anayesalia na timu nchini Hispania, Ufaransa au England kuliko kuelewa ukubwa wa mafanikio soka la Afrika.”

Upande mwingine wa benchi, Santos amepitia safari tofauti lakini yenye changamoto sawa.

Aliteuliwa kuinoa FAR Rabat Februari 2025 na ameisaidia kufika fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 1985 walipotwaa taji hilo. Safari yake katika soka la Afrika ilianza kujulikana zaidi kupitia kazi yake na Petro de Luanda nchini Angola, ambako alipata matokeo makubwa ya kimataifa.

Santos anaifahamu vyema Sundowns. Timu yake ya Petro de Luanda iliwaondoa kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2021-22.

Makocha hao wanakutana katika fainali itakayoacha hisia tofauti baina yao.

Katika hali hii, mmoja wetu atahuzunika, lakini hiyo ndiyo soka, hiyo ndiyo maisha,† alisema Santos. “Ni furaha kucheza dhidi ya Cardoso.

Sundowns wa Cardoso wamejengwa juu ya umiliki wa mpira, udhibiti wa mchezo na mashambulizi yaliyopangwa vizuri. Tangu achukue timu Desemba 2024, ameendelea kuhifadhi utambulisho wa klabu huku akiongeza nidhamu ya kiufundi na kasi ya ushindani.

Ushindi wao katika mchezo wa kwanza mjini Pretoria unawapa faida kubwa. Hawalazimiki kushambulia kwa pupa Rabat, jambo litakalowaruhusu kudhibiti kasi ya mchezo na kutumia uzoefu wao wa kucheza fainali.


Lakini FAR Rabat wana sababu ya kuamini kuwa pambano bado liko wazi.

Kikosi cha Santos kimejengwa juu ya mpangilio mzuri, uthabiti na usimamizi bora wa mchezo. Safari yao ya kufika fainali haikujengwa kwenye soka la burudani, bali uwezo wa kustahimili presha na kutumia nafasi chache muhimu.

Wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki wenye hamasa kubwa wa Morocco, FAR wanatarajiwa kucheza kwa nguvu na kasi zaidi. Wanahitaji kufunga, lakini lazima wajihadhari wasiachie nafasi nyingi kwa Sundowns ambao wana uwezo wa kuadhibu makosa.


Uwiano huo unaweza kuamua fainali.

Kwa Sundowns wanahitaji kufunga bao moja Rabat litawalazimisha FAR kuhitaji mabao matatu. Kwa miamba hiyo ya Morocco, bao la mapema linaweza kubadili kabisa mazingira ya mchezo na kuweka presha kwa wageni.

Lakini simulizi nzuri ni alama ya makocha wa Kireno katika soka la Afrika.

Kuanzia Manuel Jose akiwa Al Ahly hadi Carlos Queiroz akiwa na timu za taifa za Afrika, pamoja na Jose Morais hadi sasa kwa Cardoso na Santos, makocha wa Kireno wamekuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya soka la bara.