Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hervé Renard ajutia uamuzi wa kuiacha Morocco

HERVE Pict

Muktasari:

  • Renard, ambaye kwa sasa anaiendeleza timu ya taifa ya Saudi Arabia, aliachana na Morocco baada ya kuondolewa katika hatua ya mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2019), pale timu hiyo ilipofungwa na Benin.

Kocha raia wa Ufaransa, Hervé Renard, amekiri kuwa kujiuzulu kwake kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Morocco mwaka 2019 ilikuwa ni uamuzi wa makosa kwani alipaswa kuendelea hadi mwisho wa mkataba wake 2022.

Renard, ambaye kwa sasa anaiendeleza timu ya taifa ya Saudi Arabia, aliachana na Morocco baada ya kuondolewa katika hatua ya mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2019), pale timu hiyo ilipofungwa na Benin.

Akizungumza kwenye jukwaa la Colin Interview kupitia YouTube, Renard alisema: "Nilipaswa kubaki na timu ya taifa ya Morocco. Niliishi Morocco kwa miaka mitatu na nusu, niliiacha timu ikiwa sehemu ya moyo wangu. Nilipaswa kuendelea hadi mwisho wa mkataba wangu mwaka 2022."

Wakati wa kipindi chake na Morocco, Renard aliongoza timu hiyo kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018, akimaliza kipindi cha miaka 20 bila kushiriki mashindano hayo makubwa. 

Akikumbuka uamuzi wake wa kuondoka mapema, kocha huyo amesema uzoefu alioupata baada ya kuachana na Morocco umethibitisha kuwa uamuzi huo haukuwa sahihi.

"Nilichokiona baada ya kuondoka Morocco kimenithibitishia kuwa uamuzi wangu haukuwa sahihi," amesema Renard, akiongeza kuwa bado ana uhusiano wa kihisia na timu hiyo.

Amefafanua: "Niliipigia makofi timu ya taifa ya Morocco dhidi ya Ufaransa katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022."

Kauli hizi zinaonyesha jinsi Renard anavyothamini mchango wake kwa soka la Morocco, huku akikiri kuwa kuacha nafasi hiyo kabla ya wakati kulikuwa ni uamuzi wa majuto.