Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya sasa... Arteta amepata dawa

Arteta Pict

Muktasari:

  • Havertz, 25, ndiye mchezaji mwenye mabao mengi zaidi (15) kwa Arsenal aliyofunga katika mechi 24 za michuano yote.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amekiri anaweza kufanya uamuzi mkubwa juu ya nani atachukua nafasi ya Kai Havertz katika safu yao ya ushambuliaji.

Havertz, 25, ndiye mchezaji mwenye mabao mengi zaidi (15) kwa Arsenal aliyofunga katika mechi 24 za michuano yote.

Hata hivyo, staa huyu atakuwa nje ya uwanja kwa muda baada ya kuumia nyama za nyuma ya paja wakati  timu hiyo ilipokuwa ikifanya mazoezi huko Dubai.

Ijumaa ya wiki iliyopita, Arsenal katika tovuti yao ilithibitisha atahitaji upasuaji kutokana na jeraha hilo.

“Tulikuwa na kambi nzuri huko Dubai,  tulipokuwa tukifanya mazoezi na kupumzika kidogo katika mazingira tofauti, kisha jeraha likatokea kwa namna ambayo hatukutarajia, alikuwa anataka kuzuia shuti baada ya kona, kisha akachezesha kidogo mguu wake,” alisema Arteta kuhusiana na majeraha ya Kai.

Moja ya maswali ya kwanza yaliyoulizwa na mashabiki lilikuwa, ‘Nani atachukua nafasi yake?’

Wakati Arsenal ilipoishinda 2-0 dhidi ya Leicester City, Jumamosi, Arteta, mwenye umri wa miaka 42, alimuanzisha Raheem Sterling katika nafasi hiyo.

Hata hivyo, hakufanya vizuri na alibadilishwa na Mikel Merino aliyeingia dakika ya 69 na kufunga mara mbili na Arsenal kupata ushindi.

Lakini kabla ya mchezo, Arteta alifichua alikuwa akifikiria chaguo lingine la kuongoza safu ya ushambuliaji.

Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Martin Keown, ambaye alikuwa sehemu ya timu ya matangazo ya TNT Sports, alikiri Arteta alikuwa akimtazama Riccardo Calafiori kama chaguo linaloweza kutumika katika maeneo ya ushambuliaji.

Baadaye Arteta aliulizwa ikiwa ni kweli anamfikiria staa huyo kama mbadala katika safu ya ushambuliaji akasema:

“Imekwishafanyika hapo awali, ana uwezo huu wa kuwa tishio, hasa katika nyakati tunazokutana na timu yenye wachezaji wengi kwenye boksi na yenye kujilinda sana, yeye (Calafiori) ni chaguo ambalo tunalo.”

Kwa kawaida, Calafiori, mwenye umri wa miaka 22, anacheza kama beki wa kushoto/beki wa kati, lakini ameonyesha uwezo wa kucheza katika eneo la ushambuliaji msimu huu.

Mchezaji huyu wa Italia alifunga goli la mbali la kushangaza wakati Arsenal ilipotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Manchester City, Septemba mwaka jana na hivi karibuni alifunga bao pekee la ushindi katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Wolves Januari 25.