Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Havertz yupo tayari kwa kazikazi Arsenal

Muktasari:

  • Staa huyo wa Kijerumani amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti, lakini sasa ameonekana kurudi uwanjani na alifanya mazoezi London Colney kabla ya chama lake la Arsenal kukabiliana na Crystal Palace kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Ligi.

LONDON, ENGLAND: FOWADI wa Arsenal, Kai Havertz anaendelea vyema kupona majeraha yake yaliyotokana na kufanyiwa upasuaji wa goti ambalo lilimfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Staa huyo wa Kijerumani amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti, lakini sasa ameonekana kurudi uwanjani na alifanya mazoezi London Colney kabla ya chama lake la Arsenal kukabiliana na Crystal Palace kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Ligi.

Baada ya kucheza kwenye mechi ya kwanza ya msimu dhidi ya Manchester United, Havertz alikumbana na changamoto ya maumivu ya goti, ambayo yalihitaji upasuaji mdogo.

Na alitarajiwa kurudi uwanjani mwishoni mwa Novemba au mwanzoni mwa Desemba, lakini aliendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kuliibuka wasiwasi wa Havertz kuwa na tatizo jingine kwenye harakati zake za kupona, lakini Arteta alionekana kuzipuuza taarifa hizo kabla ya mechi ya ushindi dhidi ya Everton, Jumamosi iliyopita.

Akimzungumzia Havertz, kocha huyo wa Arsenal alisema: “Anaendelea vizuri na ameonekana kuwa fiti kwa haraka sana kwa wiki chache za karibuni. Tumekuwa na imani kubwa na kama mambo yataendelea hivi, basi atakuwa kwenye mipango.”

Havertz kurudi katika kipindi hiki kunamfanya kocha Arteta kupata mzuko wa kutosha kutokana na ukweli anahitaji kikosi chake kuwa na mastaa wengi waliofiti ili kufikia matarajio yao ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Arsenal imekumbwa na janga la majeraha kwa siku za karibuni kuanzia kwa Gabriel Magalhaes, Cristhian Mosquera, Ben White na Max Dowman.