Hatimaye Arteta asema kitu kuhusu Partey
Muktasari:
- Partey anakabiliwa na mashtaka matano ya ubakaji huku moja likiandikishwa Julai 4, siku nne baada ya mkataba wake kufika kikomo huko Arsenal.
LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema tena kwa msisitizo kwa asilimia 100 anaamini klabu yake ilifuata utaratibu wote unaofaa wa kuhusu kesi inayomkabili kiungo wa Ghana, Thomas Partey.
Partey anakabiliwa na mashtaka matano ya ubakaji huku moja likiandikishwa Julai 4, siku nne baada ya mkataba wake kufika kikomo huko Arsenal.
Mashtaka yake yanahusu wanawake watatu, huku ikidaiwa kufanya kosa hilo kati ya 2021 na 2022 na klabu huyo wa Black Stars mwenye umri wa miaka 32 atatakiwa kuhudhuria kwenye mahakama ya hakimu mkazi ya Westminster, Agosti 5.
Partey ambaye alikana kufanya makosa hayo mara ya kwanza alikamatwa Julai 2022, lakini haikuwa tatizo hivyo aliendelea kuchezea timu yake wakati uchunguzi ulipokuwa unaendelea.
Taarifa ya mwanasheria wa Partey ilibainisha: “Thomas Partey amekanusha mashtaka yote yanayomkabili. Alitua ushirikiano mzuri na polisi pamoja na maofisa wa upepelezi kwa muda wote wa miaka mitatu. Sasa anasubiri nyakati hizi muhimu za kusafisha jina lake. “Na taarifa ya klabu ya Arsenal ilisomeka: “Mkataba wa mchezaji ulifika ukomo Juni 30. Kutokana na kesi kuendelea, klabu haiwezi kusema chochote.”
Kulikuwa na maswali mengi, mojawapo kwa nini Arsenal iliendelea kumtumia Partey wakati mchezaji alikuwa na mashtaka na kuzungumzia hilo, Arteta alisema: “Klabu ilikuwa wazi kabisa juu ya jambo hilo. Kuna mambo mengi ya kisheria yenye utata, hivyo siwezi kusema kitu kingine chochote zaidi ya hilo.”