Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia 2026 tunaanza upyaaaa

32 BORA Pict

Muktasari:

  • Hadi hatua ya makundi inamalizika, tayari zimepigwa mechi 72 kati ya 104 zilizokuwa na msisimko wa aina yake katika kila kundi na sasa utamu uko hapa hatua ya 32 bora kwa maana vigogo wa soka wote wametinga hatua hii na kinachosubiriwa ni nani na nani zitapenya 16 bora.

MIAMI, MAREKANI: NDIYO. Kama alivyosema mshambuliaji wa England, Harry Kane na Kocha wake, Thomas Tuchel, Kombe la Dunia linafanana na mashindano mawili. Ya kwanza yameisha na sasa yanaingia ya pili, hatua ya 32 Bora.

Hadi hatua ya makundi inamalizika, tayari zimepigwa mechi 72 kati ya 104 zilizokuwa na msisimko wa aina yake katika kila kundi na sasa utamu uko hapa hatua ya 32 bora kwa maana vigogo wa soka wote wametinga hatua hii na kinachosubiriwa ni nani na nani zitapenya 16 bora.

Zipo timu ambazo hazikupewa nafasi zimeandika historia, kuna mbio za kiatu cha dhahabu zikiongozwa na Lionel Messi mwenye mabao sita hadi sasa na huko mtaani fainali hizi zimekuwa mjadala mkubwa na mabishano ya hapa na pale.

Hata kompyuta zilizokuwa zikifanya utabiri zilipitwa na matukio halisi, kwani timu saba kati ya nane zilizofuzu zikiwa nafasi ya tatu zilihitaji angalau pointi nne ili kufuzu 'mashindano ya pili', ambayo yanaanza leo usiku.

Hapa tunakuwekea mechi zote za hatua ya 32 ambazo hutakiwi kukosa na sababu za kuzifanya zivutie baada ya jana Afrika Kusini kuanza na Canada:

32 B 01

Kesho Jumatatu, 29 Juni

Brazil Vs Japan

Hii ni mechi kati ya vipaji vya soka dhidi ya mfumo wa nidhamu na mpangilio wa mchezo. Ni pambano linalobeba ladha halisi ya Kombe la Dunia. Brazil (Selecao) dhidi ya Samurai Blue wa Japan.

Japan, ambayo wengi wanaipa nafasi kubwa ya kufanya vizuri, iliishangaza dunia kwa kuwafunga mabingwa hao mara tano wa dunia Brazil kwa mabao 3-2 mwezi Oktoba mwaka jana.

Sasa, miaka 20 baadaye, Japan itakuwa na hamu ya kulipiza kisasi cha kipigo cha mabao 4-1 ilichopata kutoka Brazil katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia mwaka 2006.

32 B 02

Ujerumani Vs Paraguay

Paraguay itashuka dimbani dhidi ya Die Mannschaft ikiwa na dhamira ya kulipiza kisasi cha kipigo cha bao 1-0 ilichopata kutoka Ujerumani katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia mwaka 2002.

Mbali na kutafuta ushindi huo wa kulipiza kisasi, mshindi wa mechi hii huenda akakutana na Ufaransa katika hatua inayofuata ya mashindano.

32 B 03

Keshokutwa, Jumanne, 30 Juni

Uholanzi Vs Morocco

Huenda hii ikawa mechi bora zaidi wa hatua ya 32 bora. Uholanzi, ambao wengi wanawatazamia kutwaa ubingwa wa mashindano, watakutana na Morocco, waliotikisa dunia kwa kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia miaka minne iliyopita, Qatar.

Tangu wakati huo, Morocco imeimarisha kikosi chake ikiwa na kiungo chipukizi mwenye umri wa miaka 18, Ayyoub Bouaddi, ambaye anatajwa kuwa mmoja wa vipaji vinavyochipukia kwa kasi zaidi Ulaya.

32 B 04

Ivory Coast Vs Norway

Hii ni mechi ya nguvu ya wasiozuilika dhidi ya ukuta usiotikisika.

Upande mmoja yupo mshambuliaji hatari Erling Haaland, huku upande mwingine ukiwa na safu ya ulinzi ya Ivory Coast ambayo haikuruhusu hata bao moja katika mechi zake 10 za kufuzu Kombe la Dunia.

Jambo moja la uhakika ni mashabiki wa Norway wataunda burudani kubwa viwanjani kwa shangwe zao maarufu za "Viking Rowing", watakapoingia jijini Dallas kuiunga mkono timu yao.

32 B 05

Ufaransa V Sweden

Sote tunafahamu ubora na wingi wa vipaji vya safu ya ushambuliaji ya Ufaransa, lakini pambano la kuvutia zaidi katika mechi hii litakuwa upande wa ulinzi.

Macho yote yataelekezwa kwenye mpambano kati ya mshambuliaji Viktor Gyokeres na beki wa Arsenal, William Saliba. Swali kubwa ni nani kati ya nyota hawa wawili wa Ligi Kuu England atakayeibuka mshindi?

32 B 06

Jumatano, 1 Julai

Mexico V Ecuador

Kuiona Mexico ikicheza katika Uwanja wa Azteca ni burudani inayostahili kuamka mapema. Aidha, mechi hii inaweza kutoa picha ya mpinzani ambaye England anaweza kukutana naye katika hatua ya 16 bora.

32 B 07

England  V DR Congo

Tukizungumzia kikosi cha kocha Thomas Tuchel, huu ndiyo mchezo pekee wa England katika mashindano haya unaochezwa kwa muda unaofaa kwa familia nyingi kuutazama.

32 B 08

Ubelgiji V Senegal

Timu zote mbili zilionyesha kiwango chao bora katika mechi za mwisho za hatua ya makundi. Kuna dalili kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji bado kina uwezo wa kung'ara.

Kwa upande wa Senegal, licha ya kufuzu kama timu ya mwisho kati ya zilizomaliza nafasi ya tatu, walifunga mabao manane katika mechi zao dhidi ya Ufaransa, Norway na Iraq, huku changamoto zilizokuwa nje ya uwanja zikionekana kuwa zimepatiwa ufumbuzi.

32 B 09

Alhamis, 2 Julai

Marekani V Bosnia & Herzegovina

Huenda isiwe bado tarehe 4 Julai, siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Marekani, lakini wenyeji wenza wa mashindano wanaelekea katika eneo la San Francisco Bay wakiwa na morali kubwa, licha ya kupoteza kwa tofauti ndogo dhidi ya Uturuki katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ambao haukuwa na athari kwenye msimamo.

Wanakutana na Bosnia na Herzegovina, ambao walifuzu kwa gharama ya Italia mwezi Machi, lakini hawakuonyesha kiwango cha kuvutia katika hatua ya makundi.

32 B 10

Hispania V Austria

Huu unatarajiwa kuwa mchezo wa mitindo miwili tofauti ya soka.

Lamine Yamal, ambaye amerejea akiwa fiti, ataiongoza Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya dhidi ya Austria, timu inayocheza soka la moja kwa moja na la nguvu.

Austria ilifuzu kwa taabu, baada ya kupata nafasi ya kuendelea katika sekunde za mwisho za mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi, hivyo wataingia kwenye mechi hii wakiwa na imani kubwa ya kuendelea kufanya maajabu.

32 B 11

Ijumaa, 3 Julai

Ureno V Croatia

Je, huu ndio "mwisho wa enzi'?

Inaonekana ni vigumu kuamini kama Luka Modrić mwenye umri wa miaka 40 au Cristiano Ronaldo mwenye miaka 41 wataonekana tena katika Kombe la Dunia baada ya miaka minne. Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa safari ya mmoja wao katika Kombe la Dunia itafikia tamati alfajiri ya Ijumaa.

32 B 12

Uswisi V Algeria

Uswisi imecheza Kombe la Dunia mara 13 na imeishia kuondolewa kwenye hatua ya makundi mara nne pekee. Ni timu ambayo mara nyingi hufuzu hatua ya mtoano.

Hata hivyo, sasa inatafuta ushindi wake wa kwanza katika hatua ya mtoano baada ya majaribio saba yaliyopita, dhidi ya Algeria yenye nyota wa miaka 20, Ibrahim Maza, ambaye kutokana na kipaji chake kikubwa amepewa jina la utani 'Mazadona'.

32 B 13

Australia V Misri

Harakati za Mohamed Salah kuvunja rekodi ya ufungaji ya Misri ni moja ya simulizi zinazovutia zaidi katika mechi hii.

Kinachofanya hadithi hiyo kuwa ya kipekee ni rekodi hiyo inashikiliwa na kocha wake mwenyewe, Hossam Hassan. Katika mchezo uliopita, Hassan alimtoa Salah dakika 12 baada ya kuanza kipindi cha pili, wakati mshambuliaji huyo alikuwa amebakiza bao moja tu kufikia rekodi yake.

32 B 14

Argentina V Cape Verde

Mshambualiaji Messi tayari amefunga mabao sita katika mashindano haya, atakutana na kipa mkongwe wa Cape Verde mwenye umri wa miaka 40, Vozinha.

Kwa mtazamo wa karatasi, huu unaweza kuonekana kuwa mchezo wenye tofauti kubwa zaidi ya kiwango katika Kombe la Dunia. Hata hivyo, Vozinha tayari ameonyesha uwezo mkubwa kwa kutoruhusu bao katika mechi mbili na amegeuka kuwa shujaa wa taifa lake msimu huu wa mashindano.

32 B 15

Jumamosi, 4 Julai

Colombia V Ghana

Mandhari na shamrashamra za Kombe la Dunia huwa za kipekee kila wakati, na mechi hii jijini Kansas City inatarajiwa kuwa mojawapo ya zenye kuvutia zaidi.

Mechi za Colombia zimekuwa kivutio kikubwa hadi sasa, huku maelfu ya mashabiki wao wakijaza viwanja wakiwa wamevalia rangi ya njano na kuimba kwa nguvu wimbo wa taifa lao.

Mashabiki wa Ghana nao wanatarajiwa kuleta hamasa na kelele zao, hivyo kuifanya mechi hii kuwa tamasha la kweli la soka ndani na nje ya uwanja.