Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hakuna namna! Mastaa kibao kuuzwa Liverpool

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Wachezaji wakongwe wa klabu kama Mohamed Salah na Andy Robertson wanatarajiwa kuondoka wakiwa huru , lakini Slot amefunguka kuna majina mengine makubwa wataungana nao.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL inajiandaa kuuza baadhi ya wachezaji wao tegemeo dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kufidia kiasi kikubwa ilichotumia katika usajili wa mastaa kwa miaka miwili iliyopita.

Kocha wa majogoo hao wa Jiji la Liverpool, Arne Slot, ambaye  amekuwa akidaiwa huenda akafukuzwa, amesema klabu italazimika kutumia mfumo wa 'kuuza ili kununua' kwa dirisha lijalo baada ya kutumia kiasi kikubwa cha Pauni 450 milioni miaka miwili iliyopita.

Wachezaji wakongwe wa klabu kama Mohamed Salah na Andy Robertson wanatarajiwa kuondoka wakiwa huru , lakini Slot amefunguka kuna majina mengine makubwa wataungana nao.

Dirisha lililopita la majira ya kiangazi, Liverpool ilisajili nyota kama Alexander Isak, Florian Wirtz, Jeremie Frimpong na Milos Kerkez kwa gharama kubwa, hali inayosababisha sasa kuhitaji mauzo ya wachezaji wakubwa ili kupata fedha za usajili mpya.

Slot amesema kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao kutasaidia kifedha, lakini msimamo wa klabu unabaki kuwa ni lazima wauze kwanza kabla ya kununua.

“Tunachopigania sasa katika wiki zijazo ni hilo,” amesema Slot. "Klabu iko katika kipindi cha mpito. Tutauza wachezaji wengi ili kupata fedha na kusajili vipaji vipya."

Aidha, beki Ibrahima Konate ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, anaweza kuongeza mkataba mpya lakini mastaa wengine kama Curtis Jones na Wataru Endo wao wanahusishwa kuondoka.

Ripoti kutoka La Gazzetta dello Sport zinaeleza kipa Alisson Becker anawindwa na Juventus, huku Alexis Mac Allister naye akihusishwa na Barcelona.