Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres, Arsenal jambo limeiva

Muktasari:

  • Arsenal ilikuwa kwenye kipindi cha kufanya uamuzi juu ya straika gani wa kumchukua kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na sasa kura imeangukia kwa mkali, Gyokeres.

LONDON, ENGLAND: NDO hivyo. Arsenal imefikia patamu kwenye mazungumzo ya kumnasa straika wa mabao, Viktor Gyokeres baada ya kuamua kumchukua mkali huyo wa Sweden badala ya Benjamin Sesko.

Arsenal ilikuwa kwenye kipindi cha kufanya uamuzi juu ya straika gani wa kumchukua kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na sasa kura imeangukia kwa mkali, Gyokeres.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Mbelgiji, Sacha Tavolieri, Arsenal inahisi kama imeshafika kwenye hatua nzuri ya kukamilisha dili hilo kwa kukubaliana na straika huyo wa Sporting Lisbon.

Kinachoelezwa ni kwamba Arsenal imefikia makubaliano ya kumsainisha Gyokeres mkataba wa miaka mitano. Straika Gyokeres amejikuta kwenye hatari ya kulazimisha uhamisho baada ya mabosi wa Sporting kubadili mawazo yao juu ya makubaliano ya awali ya kumruhusu kuondoka kwa dau dogo.

Hilo limekuja baada ya rais wa Sporting, Federico Varandas kudai kwamba watakubali kumwaachia straika Gyokeres kwa dau lisilofikia bei yake anayouzwa iliyobainishwa kwenye kipengele cha mkataba wake, lakini watapambana kupata pesa nzuri kwenye kumuuza kinara wao wa mabao.

Bosi Varandas aliambia O Jogo: “Sporting haitaki kumuuza, lakini itabaki kuheshimu ndoto za Viktor na mchezaji mwingine yeyote yule. Baada ya vikao vya wiki kadhaa, hatukutana kulipwa kiwango kilichopo kwenye kipengele cha mkataba wake, lakini tutataka bei nzuri kwa Viktor. Hii leo kuna uwezekano mkubwa ataondoka.”

Mtaalamu wa masuala ya uhamisho wa wanasoka Ulaya, Fabrizio Romano alidai kwamba uamuzi wa klabu umemtibua Gyokeres kwa sababu anaona kama amesalitiwa kwenye makubaliano yao. Na kilichoelezwa ni kwamba Gyokeres aliwaambia Sporting hatarudi kufanya mazoezi kwenye timu hiyo kama itazuia mpango wake wa kuondoka.

Gyokeres alifunga mabao 39 katika mechi 33 za ligi alizocheza msimu uliopita, ikiwa ni idadi kubwa kuliko waliyofunga wachezaji wengine kwenye ligi kubwa 10 za Ulaya.

Arsenal ilikuwa ikihusishwa sana na Sesko, lakini kwa hatua nzuri waliyopiga kwenye mazungumzo ya kumnasa Gyokeres inaweza kuwafanya kuachana na mkali huyo wa Bundesliga. Arsenal ilitangaza kumsajili kipa Kepa Arrizabalaga kutoka Chelsea kwa ada ya Pauni 5 milioni, ambapo Mhispaniola huyo atakwenda kuwa msaidizi wa kipa mwingine Mhispaniola, David Raya.

Wakati huo dili za kumnasa staa wa Brentford, Christian Norgaard na Real Sociedad, Martin Zubimendi zipo kwenye hatua nzuri za kukamilika na muda wowote zitatangazwa.