Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gwiji Manchester United awachana madogo janja

GWIJI Pict

Muktasari:

  • Kutokana na hali hiyo, Robson aliamua kuchukua hatua kwa kushirikiana na mchezaji wa zamani Simon Andrews kuanzisha kampuni maalumu inayolenga kuwapa elimu ya kifedha wachezaji wenzake.

LONDON, ENGLAND: NGULI wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, Bryan Robson, amewachana wachezaji chipukizi akiwataka kuwa makini na matumizi yao ya fedha ili kuepuka ‘stresi’ baada ya kutundika daruga.

Robson, ambaye aliwahi kuwa nahodha mashuhuri wa Manchester United, amesema amechoshwa na kusikia taarifa za wachezaji wenzake wa zamani kufilisika licha ya kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yao ya soka.

Amesema baadhi ya wachezaji hao wamejikuta wakipoteza fedha zao kutokana na mawakala wa hovyo pamoja na watu wanaotumia vibaya nafasi ya umaarufu wao kuwadhulumu mkwanja ambao wanatakiwa kupata.

Nguli huyo mwenye umri wa miaka 69 alikiri kwamba hata yeye mwenyewe aliwahi kuathirika baada ya kupoteza kiasi kikubwa cha fedha, ikiwemo mradi wa hoteli nchini Canada.

Kutokana na hali hiyo, Robson aliamua kuchukua hatua kwa kushirikiana na mchezaji wa zamani Simon Andrews kuanzisha kampuni maalumu inayolenga kuwapa elimu ya kifedha wachezaji wenzake.