Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gundogan atua kumaliza dili

Muktasari:

  • Taarifa kutoka tovuti ya Dail Maily zinaeleza Gundogan atasaini mkataba wa mwaka mmoja kurejea Man City, pia kutakuwa na kipengele cha kumwongeza mwaka mwingine kama wataridhishwa na kiwango chake.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa Barcelona, lkay Gundogan tayari ametua jijini Manchester na amefanya mazungumzo na kocha wa kikosi cha Man City, Pep Guardiola ili kujiunga na timu hiyo ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuondoka.

Taarifa kutoka tovuti ya Dail Maily zinaeleza Gundogan atasaini mkataba wa mwaka mmoja kurejea Man City, pia kutakuwa na kipengele cha kumwongeza mwaka mwingine kama wataridhishwa na kiwango chake.

Mjerumani huyu ambaye pia alikuwa akihusishwa na timu za Uturuki, alifanya kikao cha dakika 50 katika mgahawa wa Tast Catala, ambao unamilikiwa na Guardiola na pembeni yao alikuwepo pia mtendaji mkuu wa Man City, Ferran Soriano, ambaye alionekana akiwasaidia mashabiki kupiga picha na Gundogan na kuwatuliza.

Mwaka jana Gundogan alijiunga na Barcelona kwa mkataba wa miaka miwili na kucheza mechi 51 msimu uliopita, huku akifunga mabao matano.

Barcelona wanaendelea kukabiliwa na matatizo ya kifedha na wameshindwa kumuingiza mchezaji mpya Dani Olmo katika mfumo baada ya kumsajili kutoka RB Leipzig, hivyo kuondoka kwa Gundogan kunaweza kuwapa nafasi ya kufanikisha hilo.

Fundi huyu ambaye anakubalika sana na kocha wa Pep alikuwa wa kwanza kusajiliwa mwaka 2016 mara tu baada ya kocha huyo kuchukua mikoba ya kuinoa Man City mwaka 2016.

Katika kipindi cha miaka nane alichohudumu kabla ya kuondoka msimu uliopita, alicheza mechi 304 akafunga mabao 60 na pasi 38, akashinda mataji yote makubwa ikiwa pamoja na Ligi ya Mabingwa, mataji matano ya Ligi Kuu, mawili ya Kombe la FA na manne ya Carabao.

Ikiwa atatua atakuwa mchezaji wa pili  kusajiliwa na Man City dirisha hili baada ya Savinho kutoka Troyes.