Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola: Wanatuombea mabaya

Muktasari:

  • Rais wa La Liga, Javier Tebas alidai amefanya mazungumzo binafsi na klabu nyingine za Ligi Kuu England, ambao wamefichua dhamira ya kuona Man City inakumbana na adhabu ya kufanya udanganyifu kwenye matumizi ya pesa.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema wapinzani wao kwenye Ligi Kuu England wanawaombea mabaya wakutwe na hatia juu ya mashtaka yanayowakabili kwenye ishu ya kuzidisha matumizi ya pesa kwenye soka.

Man City inakabiliwa na mashtaka 130 ya kuzidisha matumizi ya pesa kwenye michuano ambayo yalianza kusikilizwa Jumatatu, huku kocha Guardiola akiamini timu nyingine 19 ziliobaki kwenye Ligi Kuu England zinawaombea mabaya wakutwe na hatia.

Rais wa La Liga, Javier Tebas alidai amefanya mazungumzo binafsi na klabu nyingine za Ligi Kuu England, ambao wamefichua dhamira ya kuona Man City inakumbana na adhabu ya kufanya udanganyifu kwenye matumizi ya pesa.

Guardiola aliulizwa kuhusu maneno hayo ya Tebas – ambaye kwa miaka mingi amekuwa akikosoa matumizi ya pesa yanayofanywa na Man City kwa miaka ya karibuni na kusema anakubaliana naye juu ya mtazamo wa wapinzani wao kwenye ligi.

“Pengine yupo sawa na timu zote za Ligi Kuu England zinahitaji jambo hilo,” alisema Guardiola.

“Nakubaliana na Tebas kwa mara ya kwanza na ya mwisho. Na ndio maana nasema, Mr Tebas na timu za Ligi Kuu England wanapaswa kusubiri tu uamuzi wa kamati huru. Najua watu wanachosubiri, najua wanachotarajia kwa sababu nafahamu hilo kwa miaka mingi, lakini kama ninavyosema mara zote kila mtu hana hatia hadi itakapothibitishwa hivyo. Haki ni demokrasia ya sasa, hivyo tusubiri uamuzi.

Mashtaka hayo yanayoikabili Man City yamefanywa kwa miaka tisa kutoka 2009 hadi 2018, huku adhabu inayoweza kuwakabili wakikumbwa na hatia ni kupokwa pointi na faini.