Guardiola aihofia West Ham

Guardiola, Solskjaer wanakutana tena uso kwa uso

MANCHESTER, ENGLAND
KOCHA wa West Ham United Pep Guardiola, amesema mchezo wao dhidi ya West Ham utakua mgumu kwa sababu ni moja kati ya timu bora kwa kuangalia nafasi wanayoshika kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Guardiola amesema licha ya upinzani uliopo kwenye nafasi nne za juu wababe hao wamefanikiwa kukaa kwa muda mrefu hivyo ni jambo la kuheshimu.
Mechi yao inatarajiwa  kupigwa saa 9:30 mchana katika dimba la Etihad ambapo Man City itahitaji kuendeleza rekodi yake ya kushinda mechi 19 mfululizo.
"Wapo kwenye nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa, hii inakuonyesha ni jinsi gani wamekua bora. Kitu ambacho nimekigundua kwao ni muunganiko wao wa timu umezidi kuimarika,"
"Wana mchezaji bora kama Declain Rice ambaye binafsi namhusudu sana kutokana na uchezaji wake, pia kuna Michail Antonio ambaye mikimbio yake ni mongoni mwa mambo ambayo yanawapa mabeki wengi maumivu ya kichwa kwa kufikiria,"aliongeza.
"Nakumbuka mechi yangu ya kwanza nikiwa na Man City nilicheza na Sunderland na wakati huo David Moyes ndio alikua kocha mkuu wa kikosi nafahamu sana juu ya ubora aliokua nao."
Kwa sasa Man City ndio kinara wa Ligi Kuu ikiwa na alama 59 baada ya kucheza mechi 25, wakati West Ham inashika nafasi ya nne ikiwa na alama 45 baada ya kucheza mechi 25.