Gomez njia nyeupe Man City

MANCHESTER, ENGLAND. MANCHESTER City imeripotiwa kukubali ada ya uhamisho wa Pauni 12.6 milioni kwaajili ya beki wa Anderlecht, Sergio Gomez.
Pep Guardiola amemtolea macho beki huyo kama mbadala wa Oleksandr Zinechenko, aliyetimkia Arsenal kwani mpango wake ni kuimarisha safu ya ulinzi.
Man City ilimuibukia Gomez baada ya kuikosa saini ya Marc Cucurella aliyesajiliwa na Chelsea kwa kitita cha Pauni 62 milioni kwa mujibu wa Fabrizio Romano.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England walimlipa Zenchenko kitita cha Pauni 12.6 kutokana na huduma yake. Kuondoka kwa beki huyo kutampa nafasi Gomez kuziba pengo lake.
Gomez atakuwa mchezaji wanne kusajiliwa na Guardiola baada ya ujio wa Erling Haaland, Kalvin Phillips na Stefan Ortega.