Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ghana, yailiza Panama dakika za jioniii, yatunza ahadi kwa Rais

Muktasari:

  • Bao la kiungo Caleb Yirenkyi dakika ya 90+5  akipokea asisti nzuri ya mshambuliaji Thomas Asante ambaye alitangulia kuwatoka mabeki wa Panama na kuweka pasi safi ya upendo, likatosha kuipa Ghana ushindi huo muhimu.

Ghana imefanya kweli baada ya kuichapa Panama kwa ushindi wa bao 1-0, huku bao lililoamua mchezo huo likipatikana dakika za mwisho za mechi hiyo.

Bao la kiungo Caleb Yirenkyi dakika ya 90+5  akipokea asisti nzuri ya mshambuliaji Thomas Asante ambaye alitangulia kuwatoka mabeki wa Panama na kuweka pasi safi ya upendo, likatosha kuipa Ghana ushindi huo muhimu.

Panama ambayo ilitawala vizuri mchezo huo itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kuzitumia nafasi hizo huku ikija kuruhusu bao katika dakika ya Tano kati ya sita za nyongeza.

Bao hilo linakuwa la sita kwa Ghana kwa ujumla kwenye ushiriki wake kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambapo katika mechi 16 ilizocheza, imepoteza saba na kutoa sare tatu.

Ushindi huo wa Ghana, unakuwa wa pili kwa timu za Afrika, ikiungana na Ivory Coast ambayo nayo ilitangulia kushinda kwa kuichapa Ecuado kwa bao 1-0, mchezo uliopigwa Juni 15,2026.

Panama baada ya kuruhusu bao hilo ikapoteza nafasi nyingine nzuri dakika ya 90+6, kichwa Cha Ismael Diaz lakini kipa akapangua na kwenda kurudi kudaka tena.

Kocha wa Ghana Carlos Queiroz, huo unakuwa ushindi wake wa kwanza kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

Ushindi huo unaifanya Ghana kushuka nafasi ya pili kwenye kundi lake L linaloongozwa na England, timu hizo zikiwa zote na pointi tatu baada ya kushinda mechi moja, ambapo England mapema imetoka kuichapa Croatia kwa mabao 4-2, ikikaa juu kwa tofauti ya nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Ghana itakutana na England Juni 23 kwenye mchezo wa pili, timu hizo zilitoka kushinda mechi ya kwanza  huku Croatia ikipambana na Panama zote zikitoka kupoteza mechi ya kwanza


Watunza ahadi zao kwa Rais wa Ghana

Staa na nahodha wa kikosi cha Ghana Jordan Ayew na kocha wa Taifa hilo Carlos Queiroz ahadi yao kwa Rais wa Taifa hilo zitawekewa tiki kwa kufanya kweli baada ya kuichapa Panama kwa bao 1-0.

Saa chache kabla ya Ghana kwenda kucheza dhidi ya Panama, kwenye mchezo wa kwanza wa wa Makundi ya Kombe la Dunia, Rais wa Ghana John Mahama, aliongea na wachezaji hao kwa njia ya mtandao wa zoom moja kwa moja wakiwa kwenye ukumbu wa mkutabo wa hoteli.

Kwenye mkutano huo Jordan ndio alikuwa wa kwanza kuongea akiwawakilisha wenzake, akisema kwa kifupi kwamba timu yao ipo tayari kwenda kushinda mchezo huo.

"'Habari za jioni Rais, kwa niaba ya viongozi, makocha na wachezaji wenzangu, tunataka kukuhakikishia kwamba tupo tayari kwa hii changamoto,haitakuwa rahisi lakini tupo tayari, tunafahamu kwamba matarajio ya watu ni makubwa kwetu, tunakuhakikishia utajibunia na tutawafanya Waghana kujivunia, tutaanza kutafuta pointi tatu kwenye mchezo huu,"alisema Ayew.

Naye Queiroz raia wa Ureno alisema vijana wapo tayari pamoja na benchi lake la ufundi na kwamba anauhakika kwamba mchezo huo utakapomalizika dhidi ya Panama Rais huyo atajivunia kazi ya timu hiyo.

"Kwa niaba ya wachezaji na wasaidizi wangu,nataka nikwambie mambo machache, vijana wapo tayari na sisi sote tupo tayari,tunafahamu majukumu yetu ,Nina uhakika na najiamini kabisa kwamba mchezo huu utakapomalizika utajivunia kazi hii ya timu, watu wa Ghana watajivunia timu yao ya Taifa"alisema Queiroz.

Bao la kiungo  Caleb Yirenkyi dakika ya 90+5  akipokea asisti nzuri ya mshambuliaji Thomas Asante ambaye alitangulia kuwatoka mabeki wa Panama na kuweka pasi safi ya upendo, likatosha kuipa Ghana ushindi huo muhimu.