Gerrard aanza na ushindi Aston Villa

Gerrard aanza na ushindi Aston Villa

London. KOCHA Mpya wa Aston Villa Steven Gerrard ameanza Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Brighton.
Mabao ya Villa yalifungwa na mshambuliaji Ollie Watkins na beki Tyrone Mings dakika sita za mwisho za mchezo na kuifanya timu hiyo kupata ushindi wa kwanza baada ya kufungwa michezo mitano mfululizo.

Gerrard alianza kutumia mfumo wa 4-3-3 ambao msimu uliopita aliutumia akiwa na timu ya Rangers ya Scotland ambapo alifanikiwa kuchukua ubingwa na kuhitimisha ndoto za wapinzani wao wakubwa Celtic walichukua mara 10, mfululizo.

Ushindi huo unakuja baada ya aliyekuwa kocha Mkuu wa kikosi hicho Dean Smith kutimuliwa kutokana na mwendendo mbaya wa matokeo.

Matokeo hayo yanaifikisha timu hiyo nafasi ya 15, kwenye msimamo wakiwa na alama 13, baada ya kucheza michezo 12.