Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho atupa kijembe Man United

GENACHO Pict

Muktasari:

  • Garnacho ametimiza ndoto zake za kwenda kujiunga na The Blues kwa ada ya Pauni 40 milioni akitokea Old Trafford, mahali ambako alisukumwa nje ya kikosi na Kocha Ruben Amorim.

LONDON, ENGLAND: STAA Alejandro Garnacho amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kujiunga na Chelsea akijaribu kuwaambia Manchester United kile ambacho watakosa baada ya kutua zake Stamford Bridge.

Garnacho ametimiza ndoto zake za kwenda kujiunga na The Blues kwa ada ya Pauni 40 milioni akitokea Old Trafford, mahali ambako alisukumwa nje ya kikosi na Kocha Ruben Amorim.

Garnacho, 21, alitibuana na Amorim mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuwekwa benchi kwenye mechi ya fainali ya Europa League.

Kabla ya hapo aliwekwa benchi kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Man United dhidi ya Aston Villa katika mechi ya mwisho ya msimu kwenye Ligi Kuu England na Amorim alimwambia hayupo kwenye mipango yake kwa msimu huu.

Garnacho hajatuma ujumbe wowote wa kuaga Man United, lakini alisema kwenye mahojiano yake ya kwanza Chelsea: “Nina akili ya ushindi. Nina dhamira na matarajio makubwa. Nafiti kabisa kwenye klabu kama Chelsea, ambayo ilishinda Kombe la Dunia la Klabu.”

“Chelsea ipo juu kwa sasa na ni muhimu kupambania klabu ambayo mashabiki wanapambania. Nilitazama Kombe la Dunia la Klabu, hivyo kujiunga na mabingwa wa dunia ni kitu spesho, hiyo ina maana sisi ni timu bora duniani!

“Si kitu cha kawaida kucheza mechi nyingi kwenye umri kama wangu, lakini hilo limenisaidia sana. Kwenye umri wa miaka 21 tu tayari nimekuwa na uzoefu mkubwa wa kucheza mechi tofauti na katika viwanja tofauti.”

Garnacho alijiunga na Man United kutokea Atletico Madrid mwaka 2020 na alifunga mabao 26 katika mechi 144 alizochezea timu hiyo baada ya kuanzia kwenye akademia.