Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamba Osaka yaipiga Al Nassr, yatwaa ubingwa wa AFC

Muktasari:

  • Kichapo hicho kimeongeza muda mrefu wa Cristiano Ronaldo kusubiri taji rasmi la klabu upande wa kimataifa.

AL Nassr imekosa fursa ya kushinda taji la bara la Asia baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Gamba Osaka katika fainali ya Ligi ya Mabingwa ya AFC mjini Riyadh, Mei 16, 2026.

Kichapo hicho kimeongeza muda mrefu wa Cristiano Ronaldo kusubiri taji rasmi la klabu upande wa kimataifa.

Ronaldo hakuweza kuiongoza timu hiyo ya Saudi Arabia kupata ushindi katika moja ya usiku mkubwa wa klabu hiyo msimu huu, huku Deniz Hummet akiifungia Gamba Osaka bao dakika ya 30, ambalo limeamua mshindi.

Kichapo hicho kimeacha hasira ndani ya Al Nassr baada ya kupoteza nafasi nyingine ya kupata kombe la kimataifa.

Matokeo hayo pia yameongeza uvumi kuhusu mustakabali wa kocha mkuu wa Al Nassr, Jorge Jesus, ambaye inasemekana anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu kufuatia kumaliza vibaya.

Taji rasmi la mwisho la kimataifa ngazi ya klabu kwa Ronaldo alibeba mwaka 2018, alipoisaidia Real Madrid kushinda UEFA Champions League msimu wa 2017-18. Hilo lilikuwa taji la tano la Champions League katika maisha yake ya soka.

Tangu wakati huo, Ronaldo amecheza Juventus, Manchester United, na Al Nassr bila kushinda tena taji rasmi la kimataifa la klabu. Ingawa Al Nassr walitwaa Arab Club Champions Cup mwaka 2023, mashindano hayo hayatambuliwi rasmi na FIFA.

Fainali ya AFC Champions League Two ilikuwa nafasi muhimu kwa Ronaldo kumaliza ukame huo mrefu, lakini nafasi hiyo ilipotea tena baada ya Gamba Osaka kutumia vizuri shuti lao pekee lililolenga lango na kutwaa ubingwa.

Ingawa mafanikio ya kimataifa katika ngazi ya klabu yamekuwa magumu kupatikana katika miaka ya karibuni, Ronaldo ameendelea kupata nyakati muhimu akiwa na timu ya taifa ya Ureno.

Baada ya kushinda UEFA Euro 2016, Ureno pia walitwaa taji la UEFA Nations League mwaka 2019 na 2025.

Ronaldo bado anatarajiwa kuwa na nafasi kubwa katika kikosi cha taifa hilo kwenye Kombe la Dunia 2026.