Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Frank Sanchez afichua alivyomvunja pua Jake Paul mazoezini

SANCHEZ Pict

Muktasari:

  • Sanchez alialikwa kwenye kambi hiyo kuelekea mpambano wa Paul dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa juu, Anthony Joshua, mwezi Desemba 2025. Alikuwa sehemu ya kikosi cha mazoezi kilichohusisha pia mabondia wakubwa kama Lawrence Okolie na Jared Anderson. 

Bondia wa uzito wa juu kutoka Cuba, Frank Sanchez, amefichua kuwa alimjeruhi vibaya pua nyota wa YouTube aliyebobea kwenye ngumi, Jake Paul, wakati wa mazoezi ya ulingoni  na kusababisha afukuzwe kambini. 

Sanchez alialikwa kwenye kambi hiyo kuelekea mpambano wa Paul dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa juu, Anthony Joshua, mwezi Desemba 2025. Alikuwa sehemu ya kikosi cha mazoezi kilichohusisha pia mabondia wakubwa kama Lawrence Okolie na Jared Anderson. 

Hata hivyo, Sanchez mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4 ndiye aliyemwacha Paul akiwa na pua iliyopinda, tukio ambalo analikumbuka kwa kicheko akieleza kuwa lilimfanya arejeshwe kwao mara moja.

SANCH 01

Licha ya tukio hilo, Jake Paul (29) alifanikiwa kupambana kwa raundi sita dhidi ya Anthony Joshua (36), ingawa aliondoka ulingoni akiwa na taya lililovunjika tukio lililomlazimu kufanyiwa upasuaji mara mbili. 

Sanchez amekiri kuwa na heshima kubwa kwa Paul baada ya kuona uwezo wake wa karibu, akimsifu kwa kuwa mtu jasiri, mwenye nguvu, na mwenye mbinu nzuri za ndondi ambazo hakuwa akidhania kama anazo. 

Baada ya kupata nafuu na ruhusa ya madaktari, Paul ambaye ana rekodi ya mapambano kumi na mbili akipoteza mawili, kwa sasa anajiandaa kurejea ulingoni na tayari amemwita bondia Canelo Alvarez, ambaye ni rafiki na mshirika wa mazoezi wa Sanchez, ingawa Sanchez amesisitiza kwa kifupi kuwa Canelo ni bondia bora zaidi.

SANCH 02

Kwa upande wake, Sanchez (33) anatarajiwa kushuka ulingoni kesho Jumamosi nchini Misri kwenye pambano la utangulizi kabla ya mpambano mkuu kati ya Oleksandr Usyk na Rico Verhoeven. 

Atapambana na Mmarekani Richard Torrez (26), ambaye ana rekodi ya kutoshindwa (14-0) na alishinda nishani ya fedha kwenye michuano ya Olimpiki ya Tokyo.

Pamoja na rekodi hiyo nzuri ya Torrez, Sanchez amemshusha thamani mpinzani wake huyo akisema kuwa hana kiwango cha juu isipokuwa tu anajua kuweka shinikizo na kurusha ngumi nyingi, akimalizia kwa msisitizo kuwa mchezo huo una viwango tofauti na yeye yuko juu.