Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fowler: Liverpool? Hii haichukui tena

FOWLER Pict

Muktasari:

  • Liverpool itarejea kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England, Novemba 22 kwa kumenyana na Nottingham Forest uwanjani Anfield. Baada ya hapo itakuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven kisha itarudi kwenye ligi kucheza na West Ham, Sunderland na Leeds United.

LIVERPOOL, ENGLAND: GWIJI wa Liverpool, Robbie Fowler amebainisha sababu zake zinazomfanya aifute timu hiyo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Liverpool kwa sasa inashika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Manchester City kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Kichapo cha Etihad kimeifanya Liverpool sasa kufikisha idadi ya mechi tano kwenye ligi hadi sasa, huku ikiwa imekusanya pointi 18 katika mechi 11.

Hiyo ina maana, Liverpool imezidisha idadi ya mechi zote ilizopoteza msimu wote uliopita na ilinyakua taji hilo na ilipoteza mechi nne tu.

FOW 02

Kikosi hicho kinachonolewa na Arne Slot kimeachwa kwa pointi nane na vinara wa ligi, Arsenal, huku mechi 27 zikiwa zimebaki kabla ya kumalizika kwa msimu huu, lakini kitu ambacho inaweza kukifanya kwa sasa ni kuweka mkazo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kutokana na hilo, Fowler amebainisha imani yake kwamba pengo la pointi lililopo baina ya Liverpool na Arsenal ni tatizo kwa miamba hiyo ya Anfield kupindua meza na kutetea ubingwa.

“Kocha anaweza kuibuka na kusema mambo mengi, hawezi kusema ‘tumekata tamaa’ kwa sababu ataonekana tatizo,” amesema Fowler.

FOW 01

“Unaweza kuona ukweli wa hilo, kwa sababu kwenye historia kuna timu mbili tu zilizowahi kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kupoteza mechi sita au saba. Hivyo, kama Liverpool itataka kushinda ubingwa wa ligi kwa sasa, itapaswa kushinda kila mechi.

“Haipaswi kutoka hata sare, inapaswa kushinda zote. Hivyo, nadhani haitakuwa kwenye mbio za ubingwa.”

Liverpool itarejea kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England, Novemba 22 kwa kumenyana na Nottingham Forest uwanjani Anfield. Baada ya hapo itakuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven kisha itarudi kwenye ligi kucheza na West Ham, Sunderland na Leeds United.