Firmino bado yupo sana Anfield

Wednesday August 03 2022
firmino pic

LIVERPOOL, ENGLAND. ROBERTO Firmino, amethibitisha kuwa hana mpango wa kuondoka Liverpool, dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, amekuwa akihusishwa, kuwa anataka kuondoka Anfield baada ya ujio wa Darwin Nunez.
Imeripotiwa Juventus imetoa ofa ya Pauni 20 milioni kwaajili ya nyota huyo wa Kimataifa wa Brazil, hata hivyo ofa yao imepigwa chini.
Aidha Firmino ameweka wazi kuhusu hatima yake Liverpool “Naipenda hii timu, mashabiki na mji wa Liverpool, nataka kubaki kwa miaka mingine zaidi”
Kauli hiyo aliizungumza kupitia kituo cha Televisheni TNT Brazil. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha Firmino yupo kwenye mipango yake msimu huu.
 “Bobby ni mchezaji muhimu kwetu, kwa upande wangu kila kitu kiko sawa, sina shaka na uwezo wake” alisema Klopp.
Kikosi cha Klopp kilianza msimu wa 2022-23 kwa kuichapa Manchester City mabao 3-1 wikiendi iliyopita kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.

Advertisement