Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yapandisha bei ya tiketi Kombe la Dunia 2026

FIFA Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa katika michuano hiyo, tiketi za kushuhudia mechi hiyo ya mwisho itakayopigwa katika dimba la MetLife, Marekani, zinauzwa hadi Dola 10,990 (zaidi ya Sh28.4 milioni), ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na Dola 8,680 (zaidi ya Sh22.5 milioni) zilizotolewa Desemba mwaka jana.

ZURICH, USWISI: SHIRIKISHO la Soka Duniani, FIFA, limeongeza bei ya juu ya tiketi za fainali ya Kombe la Dunia 2026 hadi Dola 10,990 (zaidi ya Sh27 milioni za Kitanzania), hatua iliyokuja wakati wa kufunguliwa upya kwa mauzo ya tiketi yaliyokumbwa na hitilafu za mfumo.

Inaelezwa katika michuano hiyo, tiketi za kushuhudia mechi hiyo ya mwisho itakayopigwa katika dimba la MetLife, Marekani, zinauzwa hadi Dola 10,990 (zaidi ya Sh28.4 milioni), ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na Dola 8,680 (zaidi ya Sh22.5 milioni) zilizotolewa Desemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa bei mpya, tiketi za daraja la pili zimepanda hadi dola 7,380 kutoka 5,575, huku daraja la tatu zikifikia dola 5,785 kutoka 4,185.

Mashindano hayo yatakayoshirikisha timu 48 kwa mara ya kwanza yatafanyika katika miji 11 ya Marekani, pamoja na mitatu ya Mexico na miwili ya Canada, huku FIFA ikitumia mfumo wa bei zinazobadilika (dynamic pricing) kulingana na mahitaji ya soko.

Katika michezo ya hatua ya makundi, baadhi ya tiketi zilianza kuuzwa kwa mechi chache tu kati ya 72 zilizopangwa, huku michezo ya hatua ya mtoano ikiwa bado haijawekwa wazi sokoni.

Mfumo wa mauzo nao ulizua sintofahamu baada ya mashabiki wengi kuelekezwa kwenye kurasa zisizo sahihi wakati wa awamu ya mwisho ya mauzo, kabla ya FIFA kurekebisha hitilafu hiyo baadaye mchana.

Aidha, FIFA ilisema haitatoa tiketi zote kwa wakati mmoja bali zitakuwa zikitolewa kidogo kidogo hadi mashindano yatakapoanza Juni 11 hadi Julai 19.

Hatua hiyo iliibua malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa, ambapo wabunge 69 wa chama cha Demokratiki Marekani walimtumia barua Rais wa FIFA, Gianni Infantino, wakilalamikia mfumo huo wa bei.

Walidai mfumo huo unakinzana na lengo la FIFA la kufanya soka liwe jumuishi na linalofikika kwa watu wote, wakionya Kombe la Dunia 2026 linaweza kuwa ghali zaidi kuwahi kutokea kwa mashabiki.

Pamoja na lawama hizo, Infantino alitetea mfumo huo akisema mahitaji ya tiketi ni makubwa sana, akidai maombi yaliyopokelewa ni sawa na “Mahitaji ya Kombe la Dunia kwa miaka 1,000 kwa wakati mmoja.”

Hata hivyo, bado haijawekwa wazi kama mahitaji hayo makubwa yanahusisha pia tiketi za bei nafuu, huku makundi ya mashabiki yakiendelea kuonyesha wasiwasi juu ya kupanda kwa gharama na ugumu wa kumudu tiketi hizo.