Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yaondoa nyota jezi ya Misri Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Kampuni ya Puma, inayotengeneza jezi za Misri, imelazimika kufanya marekebisho ya haraka ili kufikia masharti hayo kabla ya mchezo wa kwanza.

Kampuni ya Puma, inayotengeneza jezi za Misri, imelazimika kufanya marekebisho ya haraka ili kufikia masharti hayo kabla ya mchezo wa kwanza.

Seattle, Marekani. Timu ya taifa ya Misri imelazimika kuondoa nyota saba zilizokuwa katika jezi zake za Kombe la Dunia baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuilazimisha kufanya mabadiliko hayo siku chache kabla ya mchezo wake wa kwanza wa Kundi G dhidi ya Ubelgiji.

Nyota hizo saba kwenye jezi za mafarao zilikuwa zinawakilisha mataji saba ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo Misri imewahi kutwaa, lakini kwa mujibu wa kanuni za vifaa vya mashindano vya FIFA, nyota kwenye jezi za timu za taifa zinapaswa kuhusishwa na ubingwa wa Kombe la Dunia pekee.

Ingawa Misri inatawala Afrika kwa mafanikio yake, bado haijawahi kutwaa ubingwa wa Dunia, hali iliyoifanya FIFA kuonya kuwa matumizi ya nyota saba yangeweza kuleta mkanganyiko kwa watazamaji duniani.

Aidha, FIFA pia imegusia muonekano wa majina na namba za wachezaji kwenye jezi hizo. Awali, Misri ilikuwa ikitumia maandishi ya dhahabu, lakini shirikisho hilo limepinga likisema rangi hiyo haionekani vizuri kwenye matangazo ya televisheni.

Hatimaye, iliamriwa mabadiliko ya haraka ambapo rangi ya maandishi imebadilishwa kuwa nyeupe ili kuboresha muonekano wake kwa watazamaji wa televisheni.

Kampuni ya Puma, inayotengeneza jezi za Misri, imelazimika kufanya marekebisho ya haraka ili kufikia masharti hayo kabla ya mchezo wa kwanza.

Misri itashuka dimbani kesho Jumatatu, Juni 15, 2026 katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Ubelgiji.