Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ferdinand ataja timu za ubingwa

FERDINAND Pict

Muktasari:

  • Kocha Arne Slot amekuwa na msimu wa kwanza bora kabisa kwenye kikosi cha Liverpool akibeba ubingwa wa ligi, akiizidi Arsenal kwenye mbio hizo, ikimaliza nafasi ya pili kwa msimu wa tatu mfululizo.

LONDON, ENGLAND: RIO Ferdinand ametabiri Liverpool na Manchester City ni timu pekee zenye uwezo wa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao, akiiweka kando Arsenal.

Kocha Arne Slot amekuwa na msimu wa kwanza bora kabisa kwenye kikosi cha Liverpool akibeba ubingwa wa ligi, akiizidi Arsenal kwenye mbio hizo, ikimaliza nafasi ya pili kwa msimu wa tatu mfululizo.

Man City, iliyokuwa mabingwa watetezi kwa msimu uliopita, ilimaliza msimu kwenye nafasi ya tatu baada ya kuwa na msimu wa ovyo.

Na kwenye dirisha hili la usajili, Liverpool imeshanasa mastaa kadhaa wa kuboresha kikosi chao, wakati Man City nayo ikifanya hivyo ili kuwa na nguvu kubwa msimu ujao.

Hilo linamfanya Ferdinand kuamini timu hizo ndizo zitakazoshindana kwenye ubingwa na kuiweka kando Arsenal, ambayo hadi sasa inahangaika kusajili straika wa kiwango cha dunia.

“Itakwenda kuwa vita ya Liverpool na Man City msimu ujao,” alisema Ferdinand akizungumzia mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

“Usajili wa Arsenal kwa sasa unaonekana utakuwa wa Norgaard, ambaye ana miaka 31, Kepa, ambaye alikuwa kipa wa akiba Chelsea, na Martin Zubimendi, lakini mashabiki wao wote wanalia na usajili wa straika na winga wa kushoto.”

Ferdinand amevutiwa na usajili iliyofanya Liverpool hadi sasa kwenye dirisha hili baada ya kuwanasa Florian Wirtz, Jeremie Frimpong na Milos Kerkez.

Alisema: “Nadhani kisichozungumzwa kwa sasa ni uwezo wa Liverpool kwenda kusajili mchezaji ambaye Man City ilimtaka, Bayer Munich ilimtaka na Real Madrid ilimtaka. Liverpool inaoenakanimekuja juu sana.”