Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fabregas avunja ukimya, aipa kipaumbele Como kuliko Chelsea

Muktasari:

  • Chelsea wamelazimika kuanza mchakato wa kutafuta kocha mpya baada ya kumfuta kazi Liam Rosenior, kufuatia matokeo mabaya yaliyoshuhudia timu hiyo ikipoteza michezo mitano mfululizo bila kufunga bao katika Ligi Kuu ya England.

COMO, ITALIA: ALIYEKUWA nyota wa Chelsea, Cesc Fabregas, amevunja ukimya kuhusu tetesi zinazomuhusisha na kibarua cha ukocha katika klabu hiyo huko Stamford Bridge, akisisitiza kuwa kwa sasa mawazo yake yapo Como, Italia.

Chelsea wamelazimika kuanza mchakato wa kutafuta kocha mpya baada ya kumfuta kazi Liam Rosenior, kufuatia matokeo mabaya yaliyoshuhudia timu hiyo ikipoteza michezo mitano mfululizo bila kufunga bao katika Ligi Kuu ya England.

Katika kipindi hiki cha mpito, Calum McFarlane amepewa jukumu la kuiongoza timu kwa muda, akianza na mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Leeds United.

Fabregas, ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika kazi yake ya kwanza ya ukocha akiwa Como, ametajwa kuwa miongoni mwa majina yanayoweza kuchukua nafasi hiyo kubwa Chelsea.

Hata hivyo, kiungo huyo wa zamani wa Hispania, amesema wazi kuwa kwa sasa hana mpango wowote wa kuondoka Italia.

“Kwa kweli hakuna cha kusema kuhusu hilo. Itakuwa ni ujinga kufikiria mambo hayo sasa. Kipaumbele changu ni mchezo ujao dhidi ya Genoa,” amesema Fabregas.

Ameongeza: “Ninaamini nitaendelea kuwa kocha wa Como na nataka kumaliza msimu huu vizuri. Ningekuwa na wazimu kama ningefikiria jambo lingine tofauti na mechi hizi zilizobaki na kuhakikisha tunafuzu kwenda Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu.”

Fabregas pia ameeleza kuwa hajasikia kauli za mmiliki wa Como, Mirwan Suwarso, ambaye alieleza kuwa mchezaji huyo wa zamani yuko huru kwenda Chelsea endapo atataka.

Mmiliki huyo alinukuliwa akisema kwamba ingawa wanamthamini sana, hawawezi kumzuia endapo atapata ofa ya kwenda Stamford Bridge.

Kauli hiyo imeongeza moto katika uvumi unaoendelea kuhusu hatma ya Chelsea, ambao sasa wako katika kipindi kigumu cha kujijenga upya baada ya msururu wa matokeo mabaya.

Fabregas ambaye aliichezea Chelsea kati ya mwaka 2014 hadi 2019 na kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu England, anatajwa kati ya makocha ambao wanaweza kuifanya timu hiyo kuwa tishio Ulaya.