Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Evra awakaanga magwiji Man United wanaomkosoa Michael Carrick

EVRA Pict

Muktasari:

  • Beki huyo wa kushoto wa zamani wa Man United, Evra aliwakosoa Gary Neville, Roy Keane na Paul Scholes baada ya kuzua mjadala mkubwa siku za karibuni juu ya kufaa au kutokufaa kwa kocha Carrick katika mpango wa kumkabidhi jumla kiti cha ukocha huko Old Trafford.

MANCHESTER, ENGLAND: PATRICE Evra amewakosoa wachezaji wa zamani wa Manchester United kwa kile alichokiita uchambuzi wa hovyo dhidi ya kocha Michael Carrick, ambaye kwa sasa anafanya kazi ya kuinoa kwa muda miamba hiyo ya Old Trafford.

Beki huyo wa kushoto wa zamani wa Man United, Evra aliwakosoa Gary Neville, Roy Keane na Paul Scholes baada ya kuzua mjadala mkubwa siku za karibuni juu ya kufaa au kutokufaa kwa kocha Carrick katika mpango wa kumkabidhi jumla kiti cha ukocha huko Old Trafford.

Baada ya Man United kupata kichapo chao cha kwanza chini ya Carrick kwa kufungwa 2–1 na Newcastle United katika mechi ya ugenini Jumatano usiku, Scholes aliweka ujumbe mkali kwenye Instagram ambao baadaye aliufuta.

Scholes aliandika: “Michael ana kitu maalum sana. Lakini, Man United wamekuwa wakicheza vibaya katika mechi nne zilizopita. Usiku mwema.” Maoni ya Scholes yaliwashangaza baadhi ya mashabiki wa Man United, huku wengine wakiamini kuwa amekuwa mkosoaji mkubwa wa klabu hiyo kwa muda mrefu. Sasa Evra ameingilia kati, akimkosoa Scholes pamoja na Neville na Keane, ambao pia wamekuwa wakilaumiwa kwa kutoa maoni ya kukatisha tamaa.

Akizungumza na tovuti ya michezo ya kubashiri ya Stake, Evra amesema: “Natumaini posti ya Instagram ya Paul Scholes siyo yake. Natumaini akaunti yake ilidukuliwa.” Aliongeza: “Kwa kweli, sishangazwi sana na hilo kutoka kwa Scholes. Alikuwa mchezaji mtulivu zaidi niliyekutana naye katika maisha yangu yote ya soka. Lakini, sasa akiwa kwenye vyombo vya habari, anatoa kauli kali sana.”

Evra amesema pia haelewi kwa nini Carrick hapati msaada wa kutosha, aliposema: “Sielewi kabisa kwa nini hakuna msaada kwa Michael Carrick. Yeye ni mmoja wetu na anafanya kazi nzuri sana. Kumekuwa na uchambuzi hasi kutoka kwa Scholes, Roy Keane na Gary Neville.”

“Inanikasirisha kwa sababu tunataka Man United iwe kwenye nafasi nne za juu. Maoni kama hayo hayana ulazima, lakini nadhani hivyo ndivyo ilivyo unapofanya kazi kwenye televisheni – lazima uwe hasi badala ya kuwa chanya.”

Akizungumza hasa kuhusu Neville, Evra amesema: “Wengi wao wanapata kazi ya ukocha na kufukuzwa haraka. Nilimwambia Neville, ni rahisi kuongea kwenye TV. Ulipokuwa kocha wa Valencia waliomba pilau, lakini uliwapa chipsi na samaki.”

“Baada ya miezi mitatu waliamua kukuaga. Watu hawawezi kusahau walichofanya kama makocha. Kama wachezaji walikuwa magwiji, lakini kama makocha hawakufanya vizuri sana. Kwa hiyo kwao kuzungumza na pengine kuharibu taaluma ya kocha mwingine, ni jambo kubwa sana.”