Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eti tuzo ya Messi inamuuma Ronaldo

PARIS, UFARANSA. SUPASTAA, Cristiano Ronaldo ameshambuliwa na mashabiki baada ya kukomenti kwenye video ya mitandaoni inayokosoa ushindi wa Lionel Messi wa Tuzo ya Ballon d’Or usiku wa Jumatatu.

Messi alinyakua tuzo ya nane ya Ballon d’Or katika sherehe zilizofanyika jijini Paris, Ufaransa huku Ronaldo hakuwamo kabisa kwenye mchakato kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.

Ronaldo na Messi wamekuwa kwenye mchuano kwa miaka mingi, walipokuwa wakipokezana tuzo hiyo, lakini sasa ushindi wa nane kwa mkali wa Argentina unamfanya Messi aweke pengo la tofauti ya tuzo tatu na mpinzani wake huyo. Ronaldo amenyakua Ballon d’Or mara tano.

Na baadhi ya mashabiki wanadai Ronaldo ameumia kwa kuachwa sana na mpinzani wake kwenye tuzo hilo.

Baada ya sherehe hizo za Paris, Mwandishi wa Habari, Tomas Roncero alituma video akielezea tuzo hiyo.

Alisema: “Kwenu marafiki. Tunachofahamu, wanakwenda kumpa tena Messi Tuzo ya Ballon d’Or. Alikwenda kustaafu Miami, licha ya kwamba alikuwa amestaafu akiwa PSG. Alishinda Kombe la Dunia, sawa ni vizuri, lakini kwa penalti sita... Kombe la Dunia lenyewe lilifanyika miezi 10 iliyopita.

“Messi ana Ballon d’Or nane, zilipaswa kuwa tano. Ana tuzo ya (Andres) Iniesta/Xavi, ana ya (Robert) Lewandowski, ambaye alishinda mataji sita ndani ya msimu mmoja na ana ya (Erling) Haaland kinara wa mabao wa msimu.”

Ronaldo akakomenti kwenye video hiyo iliyopostiwa Instagram kwa kuwake emoji nne za kicheko chini yake.

Licha ya kwamba haifahamiki Ronaldo alikuwa na maana gani, mashabiki wamemshutumu na kudai hakupenda Messi kushinda Ballon d’Or tena.

Shabiki wa kwanza aliandika: “Siamini kabisa hii ni tabia gani, kwanini hataki kukubali kwamba mjadala umefungwa.”

Shabiki mwingine aliongeza: “Huyu jamaa hana aibu kabisa.” Shabiki wa tatu aliposti: “Ronaldo ana utoto, kuna watu wanaona ndiye mchezaji wao bora wa muda wote. Ballon d’Or ya Messi imemuuma sana.”

Messi ameshika namba moja kwenye tuzo hiyo akifuatiwa na Erling Haaland kwenye namba mbili na Kylian Mbappe namba tatu, wakati Jude Bellingham alishinda tuzo ya Kopa Trophy (kinda bora wa mwaka) na Emiliano Martinez tuzo ya Yashin Trophy (kipa bora wa mwaka).