Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Esperance yamtema kocha, kisa kichapo cha Stade Malien

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo ya Kundi D iliyochezwa Bamako uliiacha Esperance ikiwa katika hali ngumu ya kufuzu hatua ya robo gainali baada ya matumaini yao kuyumba kufuatia matokeo hayo.

KLABU ya Esperance de Tunis imethibitisha kuachana na kocha mkuu wao  Maher Al-Kanzari kufuatia kipigo cha 1-0 ilichopata ugenini dhidi ya Stade Malien katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika juzi Jumapili.

Mechi hiyo ya Kundi D iliyochezwa Bamako uliiacha Esperance ikiwa katika hali ngumu ya kufuzu hatua ya robo gainali baada ya matumaini yao kuyumba kufuatia matokeo hayo.

Kupitia taarifa rasmi kwenye mitandao ya kijamii, klabu hiyo ya Tunisia ilisema:

“Kumalizika kwa uhusiano wa kimkataba na kocha Maher Al-Kanzari.”

Benchi jipya la ufundi kutangazwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Tunisia News, Rais wa Esperance, Hamdi Meddeb, aliamua kusitisha mkataba kati ya klabu na kocha huyo.

Taarifa hiyo ilieleza pia kuwa: “Muundo wa benchi jipya la ufundi utatangazwa katika siku zijazo.”


Mapema Septemba, uongozi wa Esperance ulikuwa umeonyesha imani kwa Kanzari licha ya kupoteza mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Stade Tunisien. Huo ulikuwa ni mwanzo wa msimu wa 2025/26 uliokuwa wa kusuasua kwa klabu hiyo.

Hadi sasa, Esperance imeshinda mechi mbili tu na inashika nafasi ya nne katika  ligi ikiwa na pointi nane.

Licha ya kipigo hicho, Esperance maarufu kama Blood and Gold   bado inashika nafasi ya pili kwenye Kundi D ikiwa na pointi sita, ikishinda mechi moja tu na sare tatu.

Imefunga mabao manne na kuruhusu manne pia.
Kwa upande mwingine, Stade Malien inaongoza kundi hilo kwa pointi 11 baada ya kushinda mechi tatu na sare mbili. Imefunga mabao matano na kuruhusu bao moja tu kuonyesha ilivyo na safu mgumu ya ulinzi katika kundi hilo lenye timu za Simba na Petro Atletico pia.

Maher Kanzari aliwahi kuiongoza timu ya taifa ya Tunisia ya vijana chini ya miaka 17 kufuzu Kombe la Dunia la FIFA U-17 mwaka 2007 lililofanyika Korea Kusini, baada ya kufika nusu fainali ya AFCON U-17 mwaka huo.

Aliwahi pia kufika hatua ya 16 bora baada ya kuzifunga timu kama Ubelgiji na Marekani, jambo lililomfanya Esperance kumteua kuwa kocha msaidizi mwaka 2007.

Baada ya kuondoka kwa Faouzi Benzarti mwaka 2010, Kanzari alichukua nafasi ya ukocha wa Esperance kwa muda, kabla ya kumpisha Nabil Maâloul wiki chache baadaye.