Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Esperance, Ahly ni fainali ya kisasi

Muktasari:

  • Mchezo wa kwanza miamba hiyo ilipokutana Tunisia, hakukuwa na mbabe baada ya kutoka sare ya bila kufungana, huku mchezo huu wa leo ukibeba dhana ya kulipa kisasi kwa Esperance dhidi ya Al Ahly kutokana na matokeo ya mechi zao za nyuma zilipokutana.

MAMBO ni moto. Ule usiku wa Mabingwa wa Afrika ndo leo, ambapo kitapigwa kipute cha pili cha hatua ya fainali baina ya Al Ahly na Esperance huko Misri.

Mchezo wa kwanza miamba hiyo ilipokutana Tunisia, hakukuwa na mbabe baada ya kutoka sare ya bila kufungana, huku mchezo huu wa leo ukibeba dhana ya kulipa kisasi kwa Esperance dhidi ya Al Ahly kutokana na matokeo ya mechi zao za nyuma zilipokutana.

Esperance, ambao ni mabingwa manne wa Ligi ya Mabingwa Afrika (1994, 2011, 2018 na 2019), katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita imetolewa mara mbili na Ahly kwenye nusu fainali ya michuano hii. Hilo linaifanya Esperance kuingia uwanjani huko Cairo, ikitaka kulipa kisasi huku ikiwa na mpango wa kuitibulia Ahly isinyakue taji hilo kwa mara ya 11.

Hii inakuwa ni fainali ya tatu kuzikutanisha timu hizi katika Ligi ya Mabingwa ambapo  mara mbili zilizopita kila timu imeshinda moja.

Mchezo wa fainali ya kwanza uliopigwa  Tunisia kwenye uwanja wa Stade Hammadi Agrebi, Tunis ukahudhuriwa na mashabiki 35,000 ulimalizika kwa suluhu.

Mara ya mwisho Esperance kukutana na Ahly ilikuwa ni msimu uliopita katika hatua ya nusu fainali ambapo walitolewa kwa mabao 4-0.

Mmoja kati ya mastaa hatari waliopo Ahly ni Hussein El Shahat anayeongoza kwa utupiaji katika kikosi hicho kwa michuano hii akiwa na mabao matatu sawa na staa wa Esperance, Mbrazili Yan Sasse.