Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EPL yashauriwa kuanzisha 'Play-off' za kushuka daraja

PLAY OFF Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa jopo la ushauri wa michezo la talkSPORT linaamini EPL lazima inapaswa kutekeleza njia mpya ya kuamua ni timu gani itashuka daraja kutoka Ligi Kuu England, badala ya sasa kuwa na mashindano ambayo humalizika na kuamua nani anashuka na yupi hashuki mara tu yanapomalizika.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England inapaswa kuanzisha mechi za mchujo (play-off) za kushuka daraja ili kurudisha utaratibu uliowahi kuwapo miaka ya nyuma na hivyo kuifanya kuwa bora zaidi kwa kuwa mara tu baada ya msimu kumalizika timu kadhaa ziliopo nafasi ya chini zitapambana kutoshuka.

Hatua hiyo inaelezwa kwamba inaweza kuchochea ufanisi fulani katika maendeleo na mafanikio ya ligi sambamba kuvutia wadhamini maalumu tu kwa ajili ya mechi za kutoshuka daraja.

Ingawa hilo linaweza kuwa gumu kukubalika kwa kuwa timu 20 zinazoshiriki ligi hiyo ni wamiliki wenza wa kampuni inayoendesha michuano hiyo, lakini ni ushauri wa kishujaa ambao kama utakubalika unaweza kurejesha mfumo ambao uliwahi kuwapo kabla ya ligi hiyo kuwa Ligi Kuu 1992-93.

Kwa mujibu wa jopo la ushauri wa michezo la talkSPORT linaamini EPL lazima inapaswa kutekeleza njia mpya ya kuamua ni timu gani itashuka daraja kutoka Ligi Kuu England, badala ya sasa kuwa na mashindano ambayo humalizika na kuamua nani anashuka na yupi hashuki mara tu yanapomalizika.

Mtangazaji maarufu wa michezo wa nchi hiyo, Adrian Durham anasema: “Play-off ni nzuri, nafikiri sote tunakubaliana na hilo. Kushuka Ligi Kuu kwa kawaida ni kitu kisichovutia. Kwa hiyo tunafanyaje iwe ya kuvutia? Tunafanyaje iwe burudani? Lete ushindani mkali. Fikiria vita ya play-off wa kuanguka daraja Ligi Kuu.

“Iwapo ungeiweka msimu huu, fikiria fainali ya play-off Uwanja wa Wembley, West Ham dhidi ya Spurs mshindi anabaki, anayepoteza anakushuka.

“Hilo ni la kimataifa. Kote ulimwenguni litalivutia. Ghafla, umeleta kitu kipya na hakutakuwa na kurudi nyuma. Kwa nini mtu mwenye akili asikubali hili? Sijaelewa kwa nini bado hatujalifanikisha. Play-off za kushuka Ligi Kuu lazima ziingizwe haraka iwezekanavyo kwenye mfumo.”

Kwa kuwa West Ham iliyopo nafasi ya 18 na Tottenham Hotspur iliyopo nafasi ya 17 zina tofauti ya pointi moja pekee kabla ya michezo saba ya mwisho ya msimu, mbio za kuepuka kujiunga na Wolves na Burnley kwenda Championship zinatarajiwa kwenda hadi hatua ya mwisho.

Spurs walimteua Roberto De Zerbi Jumatano wiki iliyopita wakimpa kocha huyo Muitaliano mkataba wa miaka mitano huku wakiwa na matumaini ya kuivusha klabu hiyo kwenye janga la kushuka.

Naye Alex Crook mmoja wa waandishi wa habari mahiri wa michezo anasema kuanza kufikiria kwamba timu zishindane kutoshuka daraja sawa na inavyokuwa timu zinazoshindana kukamilisha idadi ya timu za kupanda EPL ni suala la bora na linapaswa kuwapo katika ulimwengu wa sasa.

“Nafikiri tunajaribu tu kuiangusha ligi yetu, sivyo? Unajua nini? Sio wazo mbaya sana. Msimu uliopita huo ungekuwa mchuano kati ya Spurs na moja kati ya zile timu tatu ambazo hazina uwezo ambazo ziliishia katika nafasi ya 18. Kwa hiyo nafikiri inaongeza shinikizo,” anasema mwandishi huyo.

“Hii inamaanisha hutaona hali ambapo timu tatu zinazopanda kutoka Championship mara moja zinashuka tena, kama tulivyoona misimu michache iliyopita. Zilikuwa zikifanya hivyo zamani. Kulikuwa na play-off ya kushuka au kupanda daraja, ambapo timu iliyopo chini ya Ligi Kuu inakabiliana na timu iliyopo juu ya Daraja la Pili. Nafikiri Chelsea walishuka daraja kupitia play-off kama nakumbuka vizuri.”


KANUNI YA ZAMANI

Soka la England liliwahi kuwa na wakati wake wa play-off ya kushuka daraja mwishoni mwa miaka ya 1980 na hilo liliishusha Chelsea. Wakati EFL ilipoanzisha play-offs 1987, badala ya timu nne kutoka ligi moja kucheza kila mmoja, ilihusisha timu tatu kutoka daraja la chini na timu moja kutoka daraja la juu.

Mwaka 1988, Chelsea ilishika nafasi ya 18 katika First Division na ililazimishwa kucheza fainali ya mechi mbili dhidi ya Middlesbrough. Ilifungwa kwa jumla ya mabao 2–1 na hatimaye ilishuka daraja.

Mwenyekiti wa zamani wa timu ya Crystal Palace na mwandishi wa talkSPORT, Simon Jordan, hivi karibuni alitabiri EFL itaanzisha play-off ya kushuka daraja baada ya play-off za Championship kuwa bora.

“Jambo hilo lilifanyika zamani na baadaye likasimama. Lakini ilikuwa ni timu zilizopo chini. Nafikiri ilikuwa ni timu moja karibu na chini ya Ligi Kuu au First Division ya zamani, ikicheza dhidi ya timu zilizo juu Championship. Naweza kuelewa kwa nini halikufanikiwa sana,” anasema.

“Iwapo ni kuhusu kuokoa timu za Ligi Kuu England kutoka kushuka daraja, kwangu ni wazi. Nashangaa hakuna anayeshawishi hili. Fikiria kuhusu kushuka Ligi Kuu timu tatu za mwisho zinashuka baada ya michezo 38, na hapo ndipo mara chache unapata shauku ya dakika za mwisho.

“Angalia Ligi Kuu sasa ni nadra ambapo unaweza kupata mvuto wa siku ya mwisho. Ni mfano Leeds wanaenda West Ham siku ya mwisho huenda tayari itakuwa imeamuliwa maana anayeshuka anajulikana. Ingekuwa bora ikiwa tungekuwa na shauku hadi mwisho katika kila msimu.

Msimu uliopita kulikuwa na tofauti ya alama 13 kati ya timu ya tatu kutoka chini na ya nne chini, lakini ilifahamika ni timu ipi itashuka mwisho wa siku. “Lazima tuongeze hamu ya watu kufuatilia hadi dakika za mwisho. Hakuna mtu mwenye akili atakayefikiria mafanikio ya play-off.”