Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi kubwa Ulaya kinawaka leo, kesho

Muktasari:

  • Brighton ambao wamerudi kwenye fomu nzuri ya ushindi, wanakabiliana na Liverpool ambao wanapambana kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo huku Chelsea nayo ikiwa na kibarua kama cha Liverpool itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Everton wakati huo, Fulham itacheza dhidi ya Burnley huku Leeds ikiikaribisha Brentford.

BAADA ya Manchester United kukipiga jana, Ijumaa dhidi ya Bournemouth, Ligi Kuu ya England, inatarajiwa kuendelea tena leo, Jumamosi kwa mechi nne kupigwa huku vigogo wa ligi za Italia, Ufaransa, Ujrumani na Hispania nao  wakiwa mzigoni.

Brighton ambao wamerudi kwenye fomu nzuri ya ushindi, wanakabiliana na Liverpool ambao wanapambana kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo huku Chelsea nayo ikiwa na kibarua kama cha Liverpool itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Everton wakati huo, Fulham itacheza dhidi ya Burnley huku Leeds ikiikaribisha Brentford.

Katika Ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, kutakuwa na mechi tatu lakini macho ya wengi yatakuwa kwa PSG ambayo itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Nice huku kwenye Ligi ya Ujerumani kukiwa na mechi tano, kati ya hizo, Bayern Munich itakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Union Berlin, Heidenheim itaivaa Bayer Leverkusen na Dortmund itapimana ubavu na Hamburger SV.

Kwa upande wa Ligi ya Italia kutakuwa na mechi tatu, vigogo wa ligi hiyo, AC Milan watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Torino huku Juventus wakiikaribisha

Sassuolo huku Hispania kukiwa na mechi tano, moja ya mechi kubwa na ya kutazama ni kati ya Sevilla dhidi ya Valencia.


Brighton vs Liverpool 

Brighton walikua katika hatari ya kushuka daraja mwanzoni mwa Desemba hadi Februari lakini ushindi katika mechi zao tatu kati ya nne za mwisho (Kufungwa 1), umewaondoa katika hatari hiyo. Matokeo hayo yamewafanya kufikisha pointi 40 muhimu, wakiwa nafasi ya 12 kwenye ligi na matokeo mazuri zaidi wiki hii yanaweza kuwapandisha hadi nusu ya juu ya ligi.

Hata hivyo, ushindi mmoja kati ya michezo mitano ya nyumbani ya hivi karibuni (Sare 2, Kufungwa 2) hawajawa na uhakika mkubwa wa matokeo mazuri na ukweli kwamba Manchester City ndio pekee kati ya timu tano za juu waliyopata alama dhidi yao msimu huu (Kushinda 1, Sare 1, Kufungwa 6).

Liverpool imepunguza presha kwa kocha Arne Slot kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Galatasaray katikati ya wiki, ambao umehakikisha nafasi yao robo-fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, hali hiyo ni ya muda mfupi tu ikilinganishwa na kupoteza alama muhimu katika ligi, ambapo walipata alama moja tu kati ya michezo miwili dhidi ya Wolves (walifungwa 2-1) na Tottenham (Sare 1-1).


Everton vs Chelsea

Mchezo huu unakutanisha timu mbili zinazotaka kurejea kwenye wimbi la ushindi, Everton wakitafuta kuendeleza fomu nzuri nyumbani dhidi ya Chelsea waliopoteza kasi katika mbio za kusaka nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Kwa michezo minane pekee iliyobaki, Everton wako nafasi ya nane kwenye ligi kabla ya raundi hii na nafasi hiyo inaweza kuwapa fursa ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao. Hata hivyo, kupoteza kwao kwenye mechi ya ugenini dhidi ya Arsenal wiki iliyopita (2-0) kumepunguza tofauti yao hadi alama moja tu. Watajaribu kupambania jambo lao dhidi ya timu yenye nguvu kama Chelsea huku Toffees wakiwa hawajashinda ikiwa nyumbani dhidi ya timu yoyote iliyopo katika nafasi 10 za juu msimu huu (Sare 1, Kupoteza 5).

Rekodi inaonyesha Everton wameshinda michezo mitano kati ya minane ya mwisho  nyumbani dhidi ya Chelsea (Kushinda5, Sare  2).


Nice vs PSG

Baada ya kipindi kigumu, Nice walishinda kwa mabao  2-0 dhidi ya Angers mwishoni mwa wiki iliyopita na kumaliza mlolongo wa mechi sita bila ushindi (Sare 3, Kupoteza 3). Ushindi huo umewaweka wakiwa alama nane juu ya timu tatu za mwisho. Hadi sasa, Nice hawajashinda nyumbani msimu huu tangu waliposhinda Lille Oktoba chini ya kocha wa zamani Franck Haise (Sare 4, Kufungwa 3).

PSG walipata mapumziko mwishoni mwa wiki kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea na walishinda kwa mabao 3-0 Stamford Bridge, wakishinda jumla ya mabao 8-2 na kutinga kibabe robo-fainali.

Nice wamekusanya alama 11 dhidi ya PSG katika misimu mitano iliyopita, wakishika nafasi ya tatu nyuma ya Monaco (14) na Rennes (13). Hata hivyo, PSG walishinda michezo sita kati ya minane ya ugenini (Sare 1, Kupoteza 1), wakipachika mabao kuanzia mawili katika kila ushindi wao.


Bayern Munich vs Union Berlin

Bayern Munich wanaongoza Bundesliga kwa  tofauti ya alama 9 na wanapambana kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mapema. Wababe hao wametoka kufanya balaa katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuichakaza Atalanta kwa mabao 4-1 katikati ya wiki, hivyo kushinda kwa jumla ya mabao 10-2.

Miamba hiyo ya soka la Ujerumani, inamfululizo wa michezo 11 bila kupoteza (Kushinda 9, Sare 2), ikiwa ni pamoja na ushindi wa mechi tano kwa angalau ya mabao kuanzia matatu. Hata hivyo, kupoteza alama zaidi katika kipindi cha pili cha msimu (7) kuliko kipindi cha kwanza (4) kunaonesha dalili za mapungufu lakini ushindi wao wa tano nyumbani mfululizo unatoa matumaini ya kuendelea kufanya vizuri kwa vijana hao wa Vincent Kompany.

Union Berlin, licha ya kuwa nusu ya juu katika msimamo wa Ligi ya Ujerumani, wako alama 14 mbali na nafasi ya timu sita za juu  na alama saba juu ya timu tatu za mwisho.