Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Enzo kuondoka Chelsea, Real Madrid ikichomoza

ENZO Pict

Muktasari:

  • Real Madrid imekuwa ikimfuatilia nyota huyo akiwa ni mmoja wa malengo yao pamoja na Dominik Szoboszlai wa Liverpool, lakini uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo wa Chelsea unaonekana kuwa mdogo.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa Chelsea na timu ya taifa ya Argentina, Enzo Fernandez anahusishwa kujiunga na Real Madrid baada ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

Real Madrid imekuwa ikimfuatilia nyota huyo akiwa ni mmoja wa malengo yao pamoja na Dominik Szoboszlai wa Liverpool, lakini uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo wa Chelsea unaonekana kuwa mdogo.

Vyombo vya habari vya Argentina vimekuwa vikimhusisha nyota huyo na miamba hiyo ya Hispania vikidai ataondoka Chelsea na kituo kitakachofuata ni Madrid ambako wanasaka viungo.

Inaelezwa endapoo nyota huyo atajiunga na Madrid itainufaisha pia River Plate ya Argentina, klabu aliyowahi kuichezea miaka ya nyuma.

Inaelezwa kuwa kwa sasa Enzo ndiye mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina aliyepo katika kiwango bora zaidi.

“Klabu ya England inataka kurejesha uwekezaji wake wa Euro 120 milioni na Real Madrid wako tayari kulipa kiasi hicho, lakini watalazimika kuuza baadhi ya wachezaji. River (Plate) itapata takriban Euro 5 milioni (kama mgawo wa mauzo),” ilisema taarifa ya mmoja wa waandishi mahiri wa michezo, Renzo Pantic.

Vilevile, kama ilivyoripotiwa awali na vyombo vya habari vya Ulaya mchezaji huyo anataka kuondoka England kwa sababu binafsi na kwa manufaa ya familia yake huku hali ya hewa ya nchi hiyo ikitajwa kuwa mojawapo.

Inadaiwa baridi, mvua na uhaba wa mwanga wa jua ni mambo yanayomchukiza Enzo, ambaye amezoea hali ya joto na mazingira yaliyopoa.

Februari ilielezwa anataka kufuata nyayo za rafiki yake, Julian Alvarez aliyeondoka Manchester City na kutimkia Atletico Madrid ya Hispania.

Baada ya kuona ‘La Arana’ aliweza kubadilisha maisha na kuyaboresha akiwa Madrid baada ya kujiunga na Los Colchoneros, Enzo anatamani kufanya hivyo.

Kwa upande mmoja, Alvarez alichagua kupata changamoto mpya kwengine sababu angepata nafasi chache Man City kutokana na ubora wa Erling Haaland.

Enzo anakadiriwa kuwa na thamani ya Euro 140 milioni 140 na baada ya kushinda Kombe la Dunia 2022 alinunuliwa kwa Euro 121 milioni, kiasi ambacho Chelsea waliilipa Benfica. Ikiwa Real Madrid watamsajili utakuwa ndiyo usajili ghali zaidi katika historia ya klabu hiyo.